Na Ahmed Mahmoud Arusha

JESHI la polisi mkoa wa Arusha,limewataka wanahabari nchini kutokushabikia au kuunga mkono ndoa za Jinsia moja ambayo ni vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu havikubaliki na ni kinyume cha maadili .

Rai hiyo imetolewa May 3 na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana, alipokuwa akifungua kongamano la maadhimisho ya siku ya vyombo vya habari Duniani lililoandaliwa na Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha APC kwenye ukumbi wa hotel ya Golden rose ya jijini Arusha.

Amesema kuna harakati zinazoendelea Ulimwenguni za kutaka kuungwa mkono ndoa za jinsia moja ,wanahabari wasiunge mkono vitendo hivyo na badala yake waungane pamoja kupiga vita hata kama tutatengwa na Jumuia za kimataifa vitendo hivyo ni kinyume cha maadili.

Amewataka wanahabari kutambua kuwa hakuna uhuru usio kuwa na mipaka hivyo akawataka wazingatia uzalendo katika kazi zao ili kuhakikisha habari zinazoandikwa zisiwe zinachafua nchi au mkoa na Uhuru uliopo utumike kuwalinda wanahabari wenyewe na watu wengine.

Amesema lipo tatizo la watoto kubakwa na kulawitiwa mkoani Arusha na wazazi huwa wanayamaliza kienyeji kwa kupitia vikao amesema anaomba wanahabari na wananchi kuwafichua watu wa aina hiyo na jeshi la polisi limewasha moto wa kupambana na vitendo vyote vya ukatili huo..

Amewahakikishia ulinzi wa wanahabari wanaokumbana na madhira wakati wa kutekeleza majukumu yao na kuwalinda dhidi ya vitendo vyote vya uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo wakati wa chaguzi za serikali za mitaa zitakazofanyika nchini kote mwaka huu.

Amewataka wanahabari kutokukubaliwa kutumiwa na watu wenye nia mbaya kuvuruga amani ya nchi na kusisitiza kuwa Arusha ni Geneva ya Afrika na anataka ibakie kuwa Geneva ya kweli kwa kutanguliza maslahi ya taifa mbele katika kutimiza majukumu yao ya kila siku .

Awali mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu, amesema kwa siku za karibuni kumekuwepo na migogoro kati ya wanahabari na serikali na vyombo vyake hali ambayo inaondoa uhusiano uliokuwepo na badala yake kujenga chuki .

Amesema haoni sababu ya kugombana kati ya wanahabari na serikali na vyombo vyake,na matokeo yake ni wanahabari kukamatwa na vyombo vya dola na hivyo kuibua migogoro ambayo haina ulazima.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema Jukumu la UTPC na Klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na haki .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...