Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana akizungumza na waadhishi wa habari mkoani Arusha katika siku ya Maadhimisho ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani yanayofanyika kila mwaka 3 .Mei
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa Habari Mkoani Arusha Cloud Gwandu katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Golden Rose Hotel
Victor Maleko Meneja programu kutoka Umoja wa Vilabu vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC.amesema bado hawatanyamaza hadi tujue hatma ya waandishi wa habari,bora tuendelee kupiga kelele tu.
Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa Arusha David Lyamongi akizungumza na waandishi akimuwakilisha RAC Richard Kwitega.

Baadhi ya waandishi kushoto Lilian Joel wa gazeti la uhuru na Cythia Mwilolezi kutoka gazeti la Nipashe ,wakifuatilia mambo kwa makini
Waandishi wa vyombo mbalimbali Jijini Arusha.
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano ,wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Waandishi wakifuatilia mada kwa makini
Waandishi wakifuatilia kinachoende
Waandishi wakiwa katika ukumbi wa mkutano tayari kwa kuanza kongamano la maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo ya habari duniani.
Mwandishi Abraham Gwandu akifuatilia jambo kwa makini katika kongamano la siku moja la maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari Jijini Arusha,akiwa na Seif Mangwangwi
Grace Macha mwandishi wa Tanzania Daima akiwa katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Jiji Arusha.
Kutoka kushoto ni Shaban Mdoe Katibu mwenezi wilaya ya Arumeru,Katikati Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Jijini Arusha Cloud Gwandu na Afisa programu Victor Maleko kutoka UTPC.


Na.Vero Ignatus ,Arusha.

Katika kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani,waandishi wa habari mkoani arusha wamekutana kwa pamoja ili kujadili na kuangalia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika utekelezaji wao wa ukusanyaji wa habari wa kila siku na namna yavkupata ufumbuzi.

Akizungumza mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoani hapo Claud Gwandu amesema kwa sasa kilio kikubwa cha waandishi ni kufanya kazi katika vyombo vya habari bila malipo,kukosa mikataba sambamba na kutopewa ushirikiano wakati wa utafutaji wa habari.

Gwandu amesema wanahabari wengi wanafanya kazi bila mikataba,malipo yanakuwa duni sana au hakuna kabisa, amesema, kinakosekana chama cha wafanyakazi waandishi wa habari,jambo ambalo inapelekea kutoonekana dalili za matatizo ya waandishi hayatatuliwi kwa haraka.

"Tunakosa chama cha wafanyakazi waandishi wa habari ,jambo ambalo linatupa wasiwasi kutoona wapi matatizo yetu yanashughulikuwa kwa haraka ukizingatia sisi ndiyo tunahabarisha umma,tunaelimisha,na tunaonya pia.alisema Gwandu"

Amesema waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu bila kuwa na mikataba,bila mishahara,ameviomba vyama vya utetezi wa haki za binadamu kuangalia upya swala hili dhidi ya wanahabari kufanya kazi bila kulipwa maana huo ni sawa na utumwa wa aina fulani.

Kwa upande wake Meneja Programu kutoka Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) Victor Maleko amesema kuwa hawajachoka kufanya kazi ambayo zitahakikisha kila mwandishi atakuwa sawa na kupata stahiki zake.

Ni kweli waandishi wanafanya kazi katika mazingira magumu,ya vitisho,kupotea katika mazingira ya kutatanisha,kupoteza maisha , ila hatutakaa kimya tunaendelea kupiga kelele hadi tutakapojua hatma ya waandishinwa habari alisema."UTPC kuna utaratibu tunmalizia kuuweka wa kuhakikisha kila mwanahabari anapata stahiki zake kulingana na kazi zake"

Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Jonathan Shana amewataka waandishi amewataka kuzingatia utanaduni,uzalendo,

kutumia kalamu zao vizuri,kutetea uhuru wa watu binafsi na ziwalinde wao wenyewe,na kuzilinda habari walizoziandika."Kalamu za waandishi wa habari ni silaha, zinaweza kuua, kujeruhi na kuokoa,zitumieni vizuri kwa kuilinda Amani ya nchi,uzalendo na utamaduni wa nchi yenu'' akisema Shana.

Kamanda Shana amezungumzia pia kuhusiana na haki za watoto haswa katika mkoa wa Arusha kumekuwa na wimbi la kulawitiwa na kubakwa kwa watoto ambapo kesi zake wazazi wanamalizana na wanaukoo,amesema swala hilo halitafumbiwa macho akibainika mazazi au mlezi amepewa hongo Jeshi la polisi litashughulika nae ipasavyo.

Pia amewataka waandishi kuwa mstari wa mbele kwa kutumia kalamu zao vizuri kupinga ndoa za jinsia moja ambayo ni kinyume na maadili na utamaduni wa Taifa la Tanzania kwani hata vitabu vya dini vinapinga swala hilo.

Pia amewahakikishia waandishi ulinzi na usalama wakati wa Uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na ule wa 2020. Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa(Utawala)wa,Arusha David Lyamongi ambae alimuwakilisha Katibu Tawala mkoa Richard Kwitega amesema wanatambua umuhimu na thamani ya waandishi wa habari na utendaji kazi wao.

Akijibu swali lililoulizwa na mmoja wa waandishi kuhusiana na vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi amesema kuwa mkoa wa Arusha hawapo katika muundo huo bali wameendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa hali mzuri

Amesema swala hilo la kamatakamata la waaandishi wa habari halijawekwa wazi linafanywa na uongozi wa mkoa,wilaya ,kata,amesema wataendelea kulinda haki za waandishi,amesema atapeleka taarifa hizo kwa uongozi wa mkoa kama kuna chombo chochote kile kinachoonea waandishi wa habari atoe maelekezo yake kudhibiti hali.

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo jukumu la UTPC na klabu za waandishi wa habari kuchangia uchaguzi huru na wa haki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...