Anaandika Abdullatif Yunus wa Michuzi Tv - Kagera.

Wananchi na walipa kodi Mkoani Kagera wametakiwa kuzingatia Elimu ya kodi waliyoipata katika wiki ya Elimu kwa mlipa kodi, na kuwa tayari kupokea mabadiliko mbalimbali ya kodi na usimamizi wake Kwa masilahi ya Taifa.

Wito huo umetolewa  Wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa Mlipa Kodi, ambapo Mkoani Kagera yamefanyika katika Uwanja wa Uhuru Manispaa ya Bukoba, Mei, 17 yakihudhuriwa na wananchi, wafanyabiashara, wanafunzi na wadau mbalimbali.

Katika hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera, iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi katika maadhimisho hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Ndg. Projestus Rubanzibwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera  kuendelea kutoa Elimu na Hamasa kwa Umma ili walipa kodi waendelea kulipia kodi zao sahihi na Kwa wakati, bila shurti, kutoa Elimu ya Ufahamu ya mabadiliko mbalimbali ulipaji kodi kupitia simu, matumizi ya mashine za Efds hii itachangia kwa mlipa kodi kwa mzalendo na kutimiza wajibu wake kwa maendeleo ya Taifa.

Awali akitoa salaam zake kwa niaba ya Meneja Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mkoani Kagera, amesema changamoto kubwa miongoni mwazo ni pamoja na mwitikio mdogo wa wafanyabiashara katika Elimu ya ulipaji kodi, matumizi kidogo ya EFDs, wananchi kutoomba lisiti wanaponunua bidhaa.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 13, 2019 yenye kauli mbiu ya "Karibu Tukuhudumie" yameambatana na usikilizwaji wa kero, ushauri na maoni kutoka kwa wananchi na walipa kodi, huku yakipambwa na burudani safi kutoka kikundi cha KAKAU BAND.
 Mwakilishi wa Mgeni Rasmi, Kaimu RAS-Kagera, Ndg. Projestus Rubanzibwa akionesha Risti yake aliyonunulia bidhaa, wakati akizungumza na Wananchi, wadau na walipa Kodi, kabla ya kusoma hotuba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 Sehemu ya wafanyabiashara waliohudhuria kilele cha Wiki ya Elimu kwa Mlipa kodi wakiendelea kufuatilia maadhimisho hayo katika Viwanja vya Uhuru Platform Bukoba Manispaa.
 Pichani ni maafisa Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Kagera kutoka Wilaya mbalimbali wakifuatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
 Pichani ni mfanyabiashara Ndg. John Jackson Nkwama, akiendelea kupata ufafanuzi juu ya masuala ya ulipaji Kodi kutoka kwa Afisa Kodi Mkoa wa Kagera Ndg. Fravian Mgore katika maadhimisho ya Wiki ya Elimu kwa mlipa kodi.
 Baadhi ya wananchi, wafanyabiashara na wadau wakiendelea kuhudumiwa mapema Mei 17, katika viwanja vya Uhuru Platform mjini Bukoba katika maadhimishobya Wiki ya Elimu kwa mlipa kodi.
 Pichani ni Bwn. Frank Mbeikya akitoa ushauri wake kwa Mamlaka ya Mapato Nchini juu ya kuangalia upya Kodi ya uingizwaji bidhaa nchini hasa maeneo ya Mpakani.
Kikundi cha burudani KAKAU BAND wakinogesha maadhimisho hayo kwa wimbo maalum juu ya Elimu kwa mlipa kodi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...