Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (uNIDS) Dkt. Leo Zekeng,(kulia Mwenye ) akizungumza na mtoa Muuguzi Mara baada ya kutembelea Kituo cha afya Halmashauri ya Busokelo ambacho pia kinatoa huduma za dawa kwa wagonjwa wa HIV ,kulia Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI  Tanzania (TACAIDS),Dkt.Leonard Maboko ambaye ameambatana na Mkurugenzi huyo 
 Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI  Tanzania (TACAIDS),Dkt.Leonard Maboko akizungumza na wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti Ukimwi Ngazi ya Kata Halmashuri ya Busokelo Mkoaani Mbeya.
 Wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (uNIDS) Dkt. Leo Zekeng (hayupo pichani) katika semina ya kuwajengea uwezo wajumbe hao ambayo inafadhiliwa na shirika hilo.
 Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UNIDS) Dkt. Leo Zekeng,akizungumza na  wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya (hawapo pichani) Leo Mei 20,19.




SHIRIKA la Kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa(UNAIDS), limesema ongezeko la watoto wa kike walio chini ya umri miaka kati ya 15-25 ni viashiria tosha vya uwepo wa maambukizo mapya ya virusi vya ugonjwa wa UKIMWI. 

Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika hilo, Dkt. Leo Zekeng, alipotembelea na kuzungumza na wajumbe wa kamati ndogo za kudhibiti na kupambana na UKIMWI katika Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya. 

Amesema, jamii inapaswa kutambua kuwa kitendo cha mwanafunzi wa kike kupata mimba ni viashiria tosha vya uwepo wa maambukizo ya virusi vya ugonjwa wa ukimwi hivyo jitihada zaidi zinahitajika katika kuwalinda watoto na jamii nzima. 

Aidha, ameitaka jamii kuondokana na vitendo vya kuwanyanyapaa watu wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa UKIMWI ili kupunguza kasi ya maambukizo mapya. 

“Watu wanaogopa kwenda kupima afya zao kwani wanaamini kwamba endapo watagundulika kuwa wamepata maambukizo na kuanza kutumia dawa basi jamii itawatenga, hali inayochangia kwa kiasi kikubwa kutofanikisha malengo ya serikali na mashirika binafsi ya kupunguza au kutokomeza ugonjwa huo,”amesema. 

Hata hivyo, akizungumzia hilo, Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), amesema ofisi hiyo inazitegemea sana kamati hizo katika kufikisha elimu kwa jamii kuanzia ngazi ya vitongoji, vijiji na mitaa hivyo ni vema wakajituma na kuliweka suala la UKIMWI kuwa ni agenda ya kudumu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...