Na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha.

Wananchi wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya shuhghuli za maendeleo katika vijiji vyao na sio kutegemea serikali kuwafanyia kila kitu .

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati akizindua ofisi ya kijiji cha Nsongoro kilichopo Wilayani Arumeru mkoani hapa ,ofisi iliojengwa kwa nguvu za wananchi. 

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakiacha kufanya maendeleo katika vijiji vyao kwa kudai kuwa serikali ndio inatakiwa kufanya au kuwaletea maendeleo katika vijiji vyao kitu ambacho sio cha kweli .

"napenda kutumia wakati huu kuwapon geza sana wanakijiji wa kijiji cha Nsongoro kwa hatua mliofikia ya kuuza miti ya kijiji pamoja na kujichangisha na kujenga ofisi hii ya kijiji ambayo kwa miaka yote tang mwaka 1976 mlikuwa hamna ofisi ya kijiji na mlikuwa mnatumia ofisi ya chama cha mapinduzi , unajua wananchi wengi wanafikiriaga maendeleo kama haya yanaletwaga na serikali tu kitu ambacho sio chakweli kwani wananchi pia mnaweza kufanya wenyewe vitu kama hivi”alisema Muro

Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Arumeru mwalimu Jemsi Mchembe aliwapongeza wananchi hao na kuwaambia maendeleo ya kweli yanaletwa na watu wenyewe hivyo ni vyema kila mwananchi kujituma ili kuleta maendeleo katika nchi yake na sio kutegemea tu serikali iwaletee maendeleo .

Aidha aliwaambia maendeleo pia hayana chama hivyo ni vyema wananchi kushirikiana bila kujali chama wala kabili kufanya vitu ambavyo vitawanufaisha wananchi kwa ujumla na sio wananchi wale waliopo kipini hiki pia itawasadia ata wajukuu na vitukuu watakao kuja baadae.

Naye mwenyekiti wa kijiji Cha Nsongoro alisema kuwa ofisi hiyo ya kijiji imejegwa kwa nguvu za wananchi kwa ambao walikaa na kukubaliana kuuza miti ya iliopo katikashamba la kiijiji ambapo walipouza walipata jumla ya shilingi milioni 19 na katika fedha hizo shilingi milioni 17 zilitumika kujenga ofisi hiyo ya kijiji na shilingi milioni 2 ilitumika kwa ajili kuvuna miti ilioyokuwa shambani

Wakai huo huo Baada ya kumtuhumu Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro kuamuru kushushwa kwa bendera za chadema , Wenyeviti wa vijiji vitano na vitongoji viwili wa kata ya Songoro wameamua kukihama chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) nakujiunga na chama cha mapinduzi (CCM) kwa lengo la kumuunga mkono mkuu wa wilaya ya Arumeru katika harakati zake za kuleta maendeleo.

Wenyeviti ambao Walirudi CCM ni pamoja na Eliah Mathayo Mbise aliekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Songoro,Pokeali latiaeli Nnko wa kijiji cha mulala, Sadikiel Solomon Ayo wa kijiji cha Sura pamoja na Elifasi sunguroi Nassari wa kijiji cha Kilinga.

Pia wamo wenyeviti wawili wa vitongoji Anathe Eliah mbise kitongoji cha meto kijiji cha mulala, pamoja na Sinyaeli ndetaulo mbise wa kitongoji cha kiuta kijiji cha songoro mbali na hao pia aliekuwa katibu Mwenezi wa Chadema kata ya Songoro George peter Pallangyo pamoja na mwenyekiti wa Bawacha Bi Ekael felix wamelitangaza rasmi kurudi chama cha mapinduzi hivyo Kwa sasa kata ya Songoro vijiji vyake vyote sita vimerejea chama cha mapinduzi.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea katibu wa CCM wilayani Arumeru Shabani Mdoe alisema kuwa wamefanya uhamuzi mzuri kwani wameamua kuja kuung amkoano juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro.
 Katibu tawala wa wilaya ya Arumeru Mwalimu Jemsi Mchembe akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa ofisi hiyo ya kijiji 
 Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akimpongeza moja ya mwenyekiti kwa uhamuzi aliochukuwa wa kuhamia CCM.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akifungua rasmi ofisi ya kijiji iliojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Songoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...