Na Ahmed Mahmoud,Arusha

SERIKALI imewataka wafugaji na wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia matumizi bora ya ardhi,ikiwa ni pamoja na kuepukana na uharibifu wa mazingira unasababishwa na shughuli za kibinadamu kwa lengo ya kuepukana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi.

Mkuu wa Wilaya ya simanjiro,Zephania Chaula,ameyasema hayo jana
alipokuwa akizungumza katika warsha ya siku mbili iliyofanyika jijini
hapa iliyolenga kuelimisha jamii juu ya athari za uharibifu wa
mazingira.

Amesema kuwa wakati umefika kwa jamii hususani ya wafugaji na
wakulima,kuhakikisha kuwa wanazingatia matumizi bora ya ardhi,ikiwa ni
pamoja na kulinda maliasili ya nchi hii kwa manufaa ya kizazi cha sasa
na cha baadaye.

“Nawashauri wafugaji kuhakikisha kuwa wanaboresha nyanda za
malisho,wafugaji wanatakiwa wawe na maeneo maalumu ya malisho  kwa
lengo la kuepukana na changamoto ya uharibifu wa mazingira,ikiwa ni
pamoja na kufuga mifugo michache kwa njia za kisasa na kuepukana na
tabia ya kuhamhama kwani inachangia uharibifu wa mazingira”alisema
Chaula.

Alitoa wito kwa wananchi kutumia nishati mbadala lengo likiwa ni
kuepukana na tabia ya ukataji miti ovyo kwa ajili ya kuni  na kutoa
wito kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanajenga tabia ya kupanda miti
kabla ya kukata miti.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Mradi kwa kuboresha nyanda za
mifugo na wanyamapori,Kanda ya kaskazini,kutoka shirika la TNC,Lucas
Yamati,alisema kuwa warsha hiyo ya siku mbili inawashirikisha
wakurugenzi wa halimashauri,wazee wa kimila kutoka jamii ya
wafugaji,wananchi wanaoishi katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori
pamoja na viongozi wa vijiji.

“Wengine ni wataalamu kutoka taasisi za utafiti wa
wanayamapori,mamlaka za usimamizi za wanyamapori viongozi wa serikali
na kwamba lengo la warsha hii ni kuweza kuwafanya wanajamii kuboresha
njanda za malisho,kuweka matumizi bora ya ardhi pamoja na haki za
akina mama na watoto katika katika suala zima la lishe na afya.

Amesema kuwa warsha hiyo inawaweka pamoja makundi hayo kwa lengo la
kujadili namna ya kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni
pamoja na kuwataka wakulima kuacha kulima kiholela pamoja na wafugaji
kuacha kufuga kiholela

Kwa upande wake Mjumbe  wa baraza la wanawake kutoka kata ya
Terrat,Wilayani Simanjiro, Nerikoki Charles  amesema kuwa anatarajia
kupitia warsha hiyo wao kama wafuagaji wataweza kufikia maisha bora na
wataepukana na mila potofu ikiwemo suala la mimba za utotoni na
ukeketaji.

Kadhalika aliiyomba Serikali na wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi
kuzisaidia jamii za kifugaji katika kuwajengea vituo vya afya kwani
wamekuwa wakitumia umbali mrefu kufuata huduma za afya ikiwemo baadhi yao kujifungulia njiani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...