WATU watatu, wakazi wa jijini Dar es Salaam,  wamepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka la uhujumu uchumi kwa kukutwa na nyara za serikali na utakatishaji wa vipande vinne vya meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya  Sh. Milioni 69.

Wakili wa serikali Candid Nasua amewataja washtakiwa hao kuwa ni, Godlisten Mtui, mfanyabiashara, Frank Lucas dereva wa pikipiki na Mhando Shomary, Mkulima

Mbele ya Hakimu Mkazi Maila Kasonde imedaiwa,  Mei 7 mwaka huu, huko katika eneo la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam, washtakiwa, walikutwa na vipande vinne vya meno ya tembo vya USD 30000 ambazo ni sawa na Sh. 69,025,000 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Aidha washtakiwa hao wanakabiliwa na shtaka la utakatishaji, ambapo wanadaiwa kumiliki vipande hivyo vya meno ya tembo huku wakijua wakielewa fika kuwa, vipande vivyo vya meno ya tembo vimetokana na kosa la uwindaji haramu.


Hata hivyo, washitakiwa hao hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kw kuwa, mahakama ya Kisutu  haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), atakavyoelekeza vinginevyo.

Washitakiwa wote wamerudishwa rumande hadi Juni 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...