Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.

Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imesema kuwa katika kupata maendeleo ya nchi lazima Watendaji wawajibike katika ukusanyaji wa mapato.

Hayo ameyasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Rugambwa Banyikila wakati mafunzo kazi kwa Watendaji Kata na Mitaa yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato nchini Mkoa wa Temeke kwa ajili ya uhakiki wa nyumba kwa Mkoa huo.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano katika miradi inayotekeleza asilimia kubwa inatokana na hivyo hakuna sababu ya kumuangusha Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Banyikila amesema Watendaji wa Kata na Mitaa wametakiwa kuorodhesha nyumba ili kuweka takwimu na kurahisisha katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na nyumba hizo.

Amesema TRA iko imara hivyo Manispaa itatoa ushirikiano katika zoezi la uhakiki nyumba kurahisisha ukusanyaji wa kodi ya majengo.

Nae Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Gamaliel Mafie amesema kuwa maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa watarahisha katika ukusanyaji kodi ya majengo kutokana na kuwa takwimu za nyumba.

Amesema kuwa serikali imeacha utegemezi wa misaada kwa asilimia kubwa kutokana na ukusanyaji mapato ya ndani.Mafie amesema kuwa nyumba ambazo wameuziana na kuhamisha umiliki nyumba hizo na kusomeka majina ya umiliki mpya.

Aidha amesema kodi ndio zinaendesha nchi katika miradi pamoja na utoaji wa huduma za kijamii."Kodi ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya nchi kila mtu anawajibu wa kulipa kodi ili zitumike kuleta maendeleo hayo katika huduma za kijamii"amesema Mafie.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke  Rugambwa Banyikila akizungumza na Watendaji wa Kata na Mitaa wa Halmashauri za Temeke na Kigamboni kuhusiana na Watendaji hao kuorodhesha nyumba katika maeneo hayo.
Meneja wa TRA Mkoa wa Temeke Gamaliel Mafie akizungumza na Watendaji wa Kata na Mitaa kuhusiana na uhakiki wa nyumba katika kurahisisha ukusanyaji kodi za majengo.
 Baadhi ya maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa katika mafunzo namna ya uhakiki wa Nyumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...