Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akimfafanulia jambo Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa (kulia), wakati Waziri huyo alipofika Kiwandani hapo mjini Morogoro, kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya Viongozi Wakuu wa Kampuni hiyo ambao wanadaiwa kufanyiwa vurugu na Polisi wane waliofika ofisini hapo kwa lengo la kuwakamata kwa nguvu bila kufuata utaratibu. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (katikati), akimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, wakati alipokua anatoa malalamiko yake akidai Polisi Mkoani Morogoro kuingia ndani Kiwanda chake na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu bila kufuata utaratibu viongozi wa Kampuni hiyo. Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkurugenzi wa Sheria na Uhusiano wa Kampuni ya Tumbaku Tanzania na Kiwanda cha Kusindika Tumbaku (TTPL), Richard Sinamtwa, alipokua anashirikiana na Mkurugenzi mwenzake wa Kampuni hiyo, kutoa malalamiko yao kwa Waziri huyo kuhusu Polisi Mjini Morogoro kuingia ndani Kiwanda chao na kufanya vurugu kwa kulazimisha kuwakamata kwa nguvu bila kuwa na kosa lolote.  Kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Mugabo Wekwe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...