NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 

SHIRIKA linalosaidia watu wenye maisha duni na kuleta mabadiliko chanya katika jamii  la WHO IS HUSSAIN?, kwa kushirikiana na diwani wa kata ya Vigwaza Mohsin Bharwani ,limetoa msaada wa vyakula kwa kaya 200 zilizopo kwenye kata hiyo,uliogharimu sh.milioni kumi. 

Akikabidhi msaada huo, mratibu msaidizi wa shirika la Who is Hussain?, tawi la Dar es salaam Meesam Bandali alisema,walengwa ni watu wasio na uwezo wakiwemo wenye ulemavu,wazee katika kaya 200 kata ya Vigwaza. 

"Kila kaya kati ya hizo imepatiwa box lenye vitu vilivyogharimu sh. 50,000 ,ikiwemo mchele kilo 3, maharage kilo tatu, sukari kilo 3, majani ya chai, tende na tambi ili kuwasaidia katika mwezi mtukufu wa Ramadan"alifafanua Bandali.   

Awali diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani, alilishukuru shirika hilo kwa ujali na kujitoa kwao . 

"Sisi wanasiasa tunajua hali za wananchi waliopo katika maeneo yetu ambao wana hali duni kimaisha, ikitokea wafadhili kama hawa tunashukuru, nami waliponifuata niliona ni vyema kushirikiana kusaidia baadhi ya kaya ambazo zinaishi kwenye maisha duni"alisema Bharwani. 

Nae msemaji mkuu wa Who is Hussain? Iffet Thawer alibainisha, mjukuu wa mtume Mohammad S.W.A. ambae ni Hussain , alipinga dhuluma hivyo kuwa chanzo cha wao kuhamasika kufanya shughuli za kusaidia jamii ambapo lilianza miaka kumi iliyopita huko London.
Baadhi ya wakazi waliopata msaada huo,  akiwemo Said Imani, Maimuna Iddi  walielezea, vitu hivyo vinaweza kuwafikisha kimatumizi wiki mbili jambo ambalo litakuwa limezisogeza familia hizo kutokana na hali zao. 
Diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani, akilishukuru shirika hilo kwa ujali na kujitoa kwao . 
  Msemaji mkuu wa Who is Hussain? Iffet Thawer akiongea wakati wa utoaji wa misaada Vigwaza
 Misaada ikitelemshwa Vigwaza
Wananchi wa Vigwaza wakijipanga kupokea misaada hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...