Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi nchini kanda maalum ya Dar es Salaam kitengo cha usalama barabarani, kesho kitazindua kampeni yake ya wiki ya nenda kwa usalama katika viwanja vya kituo cha Daladala simu 2000.

Akizungumza na Waandishi wa habari kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani kanda Maalum ya Dar es Salaam Marison Mwakyoma amesema uzinduzi huo utafanyika sambamba na ukaguzi wa magari katika eneo hilo.

“tunawaalika wakazi wote wanaotumia vyombo vya moto na ambavyo vinapita barabrani kufika katika viwanja vya Simu 2000 maarufu kama Mawasiliano kwa ajili ya kupata elimu ya usalama barabarani na taratibu zingine ambazo jeshi la polisi imeziandaa"amesema Mwakyoma

Akizungumza kwa niaba ya Wasanii wa filamu nchini Mwenyekiti wa kundi la Uzalendo kwanza Steve Nyerere amesema moja ya vitu vitakavyofanyika kesho ni wasanii wote wakiongozwa na yeye watafika katika eneo hilo kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi wa magari yao.

Amesema ni jambo la aibu msanii anatembea barabarani uku gari yake ikiwa haijakaguliwa, hivyo anatoa wito kwa wakazi wa Dar es Salaam na wasaniii wote kujitokeza kwa wingi 

kwa upande wake mkuu wa kituo cha ukaguzi wa mabasi Ubungo Ins Ibrahim Samwix ametaja kuwa yeye na askari wengine wamejipanga vizuri hivyo kuwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam na wale waliokuja kutembea kujitokeza kwa wingi ili waweze kukaguliwa magari yao.
Mkuu wa Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam Marison Mwakyoma akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya wiki ya Uslama barabarani ytakayofanyika kesho jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya simu 2000 maarufu kama Mawasiliano
 Mkuu wa  Kituo cha Ukaguzi wa mabasi cha ubungo , Ibrahim Samwix akieleza jinsi walivyojipanga kufanya ukaguzi katika wiki ya nenda kwa usalama  
 Msanii wa Filamu na Vichekesho ambaye ni mwenyekiti wa kundi la Uzalendo kwanza, Steve Nyerere akizungumza uwepo wa Wasanii katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama pale mawasiliano
Mmoja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam akitoa Maoni yae juu ya wiki ya nenda kwa usalama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...