Na, Editha Edward-Tabora

Waziri wa kilimo Mhe, Japhet Hasunga amezitaka bodi zote zilizopo chini ya Wizara yake kuanza kujitathimini kama zimeshindwa kuwaondolea kero ya Rushwa kwa Wakulima zijiondoe kabla ya mwezi wa saba mwaka huu

Kauli hiyo ameitoa akiwa Wilayani Urambo Mkoani Tabora wakati wa Ufunguzi wa soko la zao Tumbaku kitaifa huku akisema Wizara hiyo ina mpango wa Kusafisha watu wote ambao Wanaojihusisha na Rushwa na kukwamisha kilimo cha zao hilo

"Mwaka huu tunaanza mabadiliko makubwa ndani ya wizara ya kilimo ili Kusafisha watu waliozoea Rushwa wakafanye kazi sehemu nyingine siyo kilimo na niwaase bodi msiegemee upande wowote ule hakikisheni mnasimamia sheria"Amesema Hasunga

Mwenyekiti wa bodi ya Tumbaku nchini (TTB) Hassan Mwakasavi ameiomba Serikali kuhakikisha inawatafutia masoko ya zao hilo ili Wakulima walime kilimo cha zao hilo wakiwa na uhakika wa masoko yasiyo na Madeni na Usumbufu

"Ombi langu kwa viongozi itendeeni haki zao la Tumbaku ili Wananchi wanufaike na zao hili kwani ni zao zuri linalo stahimili ukame "Amesema Mwakasuvi

Aidha pamoja na kukabiliwa na Changamoto mbalimbali Katika uzalilishaji wa zao la Tumbaku bado linachangia pato la Taifa kwa kuingiza Fedha za kigeni zaidi ya dola za kimarekani Milioni 195.8 Katika msimu wa kilimo cha Mwaka jana.
Waziri wa kilimo Japhet Hasunga akisititiza jambo kwenye Ufunguzi wa Zao La Tumbaku Mkoani Tabora
Pichani ni Shehena ya zao la Tumbaku likiwa kwenye ghala

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...