Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
KATIKA maisha kila mtu ana kitu anachokipenda zaidi, watu wengi hasa mashuhuri wamekuwa miongoni mwa watu wanaonunua na kubadilisha magari kama jozi za viatu huku wengi wao wakieleza kuwa ni vitu wanavyopendelea na sio kufanya maonesho kama inavyoelezwa katika mitandao ya kijamii.

Mastaa wengi wamekuwa wakionesha furaha zao kwa magari wanayomiliki akiwemo mchezaji wa Juventus Christiano Ronaldo aliyeonesha gari lake jipya la kifahari aina ya Buggati, Kanye waste pia ameonesha furaha yake baada ya kumiliki Aventador hata mtoto wa mwimbaji maarufu duniani Beyonce, Blue Ivy (3) alionekana kufurahi baada ya kumiliki Ferrari.

Kwa mujibu ya jarida la Lookers, Magari kumi ghali zaidi ni haya hapa;

10. Pagan Huayra Bc
Gari hili linauzwa Euro milioni 2.1 likiwa gari ghali zaidi zaidi kuwahi huko Italia na Horacio Pagani. Jina la gari hilo lilitolewa  a mwekezaji na rafiki wa karibu wa mtengenezaji wa gari hilo Benny Caiola, linafahamika kwa jina maarufu la "The King"

9. Ferrari Pininfarina Sergio
Gari hili linauzwa Euro milioni 2.3, na lilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kijana wa mwazilishi wa kampuni hiyo Battista Pininfarina ambaye ni Sergio Pininfarina.

Gari hili limeuzwa maeneo mengi duniani na gari ya kwanza iliuzwa katika falme za nchi za kiarabu pia katika nchi za Japan, Marekani, na Uswizi.

8. Aston Martin Valkyrie
Gari hii inauzwa Euro milioni 2.4, likiwa limetengenezwa na Aston Martini na Red Bull Racing huku matumizi ya gari hilo yakilenga kutumika kama usafiri pamoja na michezo.

7. Lykan Hypersports
Hili linauzwa Euro milioni 2.6 likiwa limeundwa na kampuni ya W.Motors kutoka Lebanon kuwa gari ya kwanza na ya kipekee kutoka Uarabuni. Na moja ya gari ya aina hii imewahi kumilikiwa na Mohammed Bin zayed Al Nahyan kiongozi wa Serikali huko uarabuni kabla ya kubadilishwa na kuwa gari ya polisi.

6. Buggati Veyron
Mansory Vivere raia wa Ujerumani ndiye aliyeunda gari hii ikiwa inauzwa kwa Euro milioni 2.7.

Ilitangazwa rasmi mwaka 2005 na kuwa gari bora na lenye nguvu mara baada ya kutangazwa sokoni na linamilikiwa na kijana mdogo wa miaka 30 Houston Crosta.

5. McLaren P1 LM
Gari hili limetengenezwa na kampuni ya magari ya Uingereza chini ya McLaren's. Likiwa na gharama ya Euro milioni 2.7 limehawi kuvunja rekodi ya gari bora mwaka 2017 kwenye moja ya mashindano ya magari.

4. Lamborghini Veneno Roadster
Linauzwa kwa Euro milioni 3.4, na hadi sasa ni magari 9 pekee yamekwisha tengenezwa huku gari moja ikiwa imeuzwa kwa Euro milioni  8 zaidi ya asilimia 200 ya bei elekezi.


3. Koenigsegg CCXR Trevita
Lilitengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009 huku ikaielezwa limetengenezwa kwa malighafi bora zaidi ikiwemo Almasi, na linauzwa  kwa Euro milioni 3.7

2. Rolls Royce Sweptail
Gari hii imefungua milango mingi ya ubunifu wa magari bora zaidi. Inauzwa Euro milioni 9.9 likiwa limenunuliwa mwaka 2013.

1. Buggati La Voiture Noire
Ni gari ghali na bora n zaidi kwa mujibu wa jarida la Lookers likiwa linauzwa Euro milioni 14.4 hadi kufikia Machi mwaka huu lilikuwa kinara kwa kuwa gari ghali zaidi, huku tetesi zikieleza kuwa mmliki wa gari hilo ni Ferdinand Piech aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni ya Volkswagen (kampuni ya magari Buggati.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...