Na Khadija seif,Globu ya jamii

MSANII wa bongomovie nchini Aunt Ezekiel amemfariji mahakamani wema sepetu.

Aunt Ezekiel ni miongoni mwa rafiki wa karibu wa msanii wema isaack sepetu na mara kadhaa wamekua wakiwa karibu kwenye shida na raha huku kupitia ukurasa wake wa Instagram akionekana kusambaza baadhi ya picha ambazo walikua pamoja huku akimuombea mazuri.

Ambapo ameonekana Leo mahakamani ya kisutu kufatia kesi iliyokua ikimkabili rafiki yake wakaribu Wema Sepetu ambaye amesota gerezani kwa siku 7 kutokana na kukiuka masharti ya dhamana.

Mahakama imemuonya msanii huyo endapo akirudia kukiuka masharti ya dhamana haitasita kumfutia kabisa dhamana hiyo.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani ambapo anadaiwa  kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, alisambaza video za ngono kupitia ukurasa wake wa Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maadili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...