Na Humphrey Shao, Kyela
Upanuzi wa bandari ya Kiwira iliyopo wilayani Kyela mkoani Mbeya unatarajia kuongeza mapato ya bandari za Ziwa Nyasa kutoka wastani wa Sh milioni 300 kwa mwaka hadi kufikia Sh bilioni 3.6.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Bandari za Ziwa Nyasa, Abeid Galus, wakati akizungunza na waandishi wa habari waliofika kuangalia Miradi ya Maendeleo inayofanywa na mamlaka ya bandari katika Ziwa Nyasa.

"Upanuzi huu unahusisha ujenzi wa sakafu ngumu katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 11,000 ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi makaa ya mawe tani 10,000 kwa wakati mmoja.  Upanuzi huo utaongeza kasi ya upakuaji wa meli tofauti na sasa ambapo meli husubiria malori yanayobeba makaa ya mawe kupeleka viwandani" amesema Galusi.

Amesema kwa sasa meli moja yenye uwezo wa tani 1000 inatumia siku tisa kushusha mzigo badala ya siku moja kama ukishushwa eneo na kuhifadhia wakati ukisubiri malori ya kuubeba.

"Ujenzi huu wa eneo la kuhifadhia mizigo utaiongezea bandari mapato kwa zaidi ya mara 100," amesema Galus.

Amesema kwa sasa bandari hiyo inahudumia wastani wa tani 5000 kwa mwaka na kiingiza mapato ya wastani wa Sh milioni 230.

"Tunatarajia baada ya upanuzi huu mwaka ujao wa fedha tutahudumia tani 72,000 kwa mwaka na kuingiza mapato ya sh bilioni 3.6,"

Aliongeza kuwa bandari hiyo pia inaongeza gati na kulifanya liweze kuhudumia meli 3 kwa wakati mmoja tofauti na sasa ambapo linahudumia meli moja tu.

Alisema miradi hiyo ambayo inahusisha pia ujenzi wa jengo la mgahawa na ofisi unagharimu bilioni 1.25 na unatarajiwa kukamilika Septemba mwakani.

Aidha Meneja huyo alisema katika kuongwza ufanisi wa huduma za bandari Mamlaka hiyo imenunu mizani mbili ambapo moja itatumika katika bandari ya Kiwira na nyingine katika bandari ya Ndumbi.

"Mizani hii itasaidia kuwa na uhakika wa uzito wa mizigo inayoingia na kutoka bandarini pia itasaidia kuongeza usalama wa vyombo vya majini kwa kutozidisha mizigo na kuondokana na kizama kwa meli," alisema Galus.

Aliongeza kuwa bandark hiyo imeongezewa vifaa vya kifanyia kazi zikiwemo mashine mbili (wheel loader) kwaajili ya kupakia na kushusha makaa ya mawe ambapo moja imepelekwa Ndumbi na nyingine imewekwa Kiwira.

Alisema pia zimenunuliwa kreni kwaajili ya kuinua vitu vizito pamoja na uwepo wa chelezo ambayo inatumika kukarabati meli za TPA pamoja na za taasisi nyingine.
 Waandishi wa Habari was vyombo mbalimbali nchini wakimsikiliza Meneja Bandari za Ziwa Nyasa Abeid Galus alipokuwa akieleezea Miradi ya Bandari za Ziwa Nyasa
 Meneja Bandari za Ziwa Nyasa,Abeid Galus akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya mafanikio yatokanayo na kuboreshwa kwa Bandari za Ziwa Nyasa.
 Meli ya Mv Mbeya ii kama inavyoonekana pichani ikiwa imekamilika kwa asilimia 85 ambapo inataraji kuanza kazi mwezi September mwaka huu.
 Sehemu ya mafundi wanaofanya marekebisho ya kuongeza Gati katika Bandari ya Kiwira Kyela Mkoani Mbeya.
Sehemu ya mafundi wanaofanya marekebisho ya kuongeza Gati katika Bandari ya Kiwira Kyela Mkoani Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...