NA MWAMVUA MWINYI,PWANI

WATU wanne wamejeruhiwa baada ya kutokea ajali ya gari la abiria aina ya higer kampuni ya Hai express huko barabara kuu ya Dar es salaam -Morogoro,eneo la Kwamatias Kibaha .

Katika ajali hiyo dereva wa gari hiyo,Juma Abdallah alitoroka baada ya kusababisha ajali kizembe ,ambapo anatakiwa kujisalimisha katika jeshi la polisi mkoani humo ,kabla hajatafutwa.

Akielezea kuhusu ajali hiyo,kamanda wa polisi mkoani ,Wankyo Nyigesa alieleza imetokea majira ya saa 1:30 asubuhi Juni 24 mwaka huu.

Alisema, gari hilo la abiria lenye namba za usajili T.329 DGC ikiendeshwa na Juma alitoroka ikiwa na abiria 48 ikitokea Dar es salaam kuelekea Mbeya,kupitia Kibaha Mji iliacha njia na kupinduka na kusababisha abiria wanne kupata majeraha.

Kati ya abiria hao watatu ni wanawake ambao wametibiwa na kuruhusiwa na mmoja mwanaume ambae anaendelea na matibabu katika hospital ya rufaa ya Tumbi .

"Chanzo cha ajali ni dereva wa gari hilo kujaribu kuyapita magari mengine barabarani katika eneo lililozuiliwa darajani hivyo kushindwa kulimudu na kuliangusha "alifafanua Wankyo.

Wankyo alibainisha ,alimtaka dereva huyo ajisalimishe mwenyewe ili achukuliwe hatua za kisheria.

Kamanda huyo aliwaasa madereva,kuacha kukiuka sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zembe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...