1. Usuli:

HAJI MANARA ni  mwanamichezo aliyetokea kwenye damu ya gozi la n'gombe. Baba yake, SUNDAY MANARA "COMPUTER" ndiye Mchezaji Bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania huku baba yake mkubwa, KITWANA MANARA "POPAT" ndiye mchezaji anaeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ya ligi, kupiga Hat-trick nyingi kuliko wachezaji wote Tanzania na aliyechezea Taifa Stars kwa muda mrefu kuliko wachezaji wote(miaka 16 toka 1960-1976) na baba yake mdogo, KASSIM MANARA, alikuwa mshambuliaji mahiri wa Taifa Stars hadi ligi kuu ya Austria.

Hata hivyo, kwa dogo wa miaka 10 aitwaye BENJAMIN "KUN" AGUERO, HAJI MANARA anasubiri sana!,  BEN aliwaacha hoi waandishi wa habari waliofurika Etihad Stadium tarehe 12 Mei 2019 siku MAN CITY ilipotwaa ubingwa wa England alipotoboa ukweli huu:

"Sergio Aguero is MY FATHER, Lionel Messi is MY GODFATHER and Diego Maradona is MY GRANDFATHER".

2. AGUERO, MARADONA & MESSI:

BEN alizaliwa tarehe 12 Februari 2009. Baba yake ni SERGIO "KUN" AGUERO, Mnyama wa MAN CITY, Mabingwa wa kabumbu England.

Mwaka 2008, SERGIO alimuoa GIANNINA, mtoto wa  DIEGO ARMANDO MARADONA, Mnyama ambaye mwaka 2000 alitunukiwa "The FIFA Player of the Century Award" pamoja na Mnyama mwingine, EDSON ARANTES D'ASCIMENTO "PELE".

SERGIO na GIANNINA wakamzaa BEN mwaka 2009. 

BEN alibatizwa mwaka 2010 ambapo baba yake wa ubatizo "Godfather" akawa ni Mnyama LIONEL ANDRES MESSI CUCCITINI wa BARCELONA.

3. BEN Akimbiza watoto wenzake:

BEN alizaliwa na kipaji cha ajabu cha kabumbu na baba yake alianza kucheza nae ndani ya nyumba akiwa na miaka miwili tu huku akionesha nguvu kubwa ya kupiga mashuti tofauti na watoto wenzake wa rika lake. Akiwa na miaka mitano akaanza kucheza na baba yake na marafiki wa baba yake kwenye garden nyuma ya nyumba ambapo aliwashangaza kwa "control" yake ya hali ya juu.

BEN alisajiliwa Man City Academy na mara moja akawa akiwakimbiza vilivyo watoto wake wa umri huo na kuwa maarufu kuliko watoto wote!.

4. SERGIO Ammwagwa na GIANNINA:

Mwaka 2012, SERGIO "KUN" AGUERO ambaye anaaminika ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuwa na mademu wengi kuliko wachezaji wote kwenye ligi ya Uingereza, alimwagwa na mkewe, GIANNINA, kutokana na kuwa na pepo la ngono!.

GIANNINA alikuwa akifumania vimeseji kwenye simu ya SERGIO na mara kwa mara akawa anashtaki kwa DAVID SILVA ambaye alikuwa akiwasuruhisha na SERGIO akiishia kuomba msamaha kwa kudai "Shetani alinipitia". Hata hivyo, mwaka 2012, GIANNINA aliporudi ghafla toka Argentina na kumfuma SERGIO akiwa na milupo miwili kwenye garden yao, MERCY TUNCAFUTZ na YACINTA FALCUM, akalianzisha vagi la kufa mtu na kusepa jumla. MARADONA alimlaani sana SERGIO kwa jinsi alivyomuumiza mwanae.

Baada ya kumwagwa, SERGIO aliendeleza weledi wake wa kutupia magoli kambani akiwa na Man City na Timu ya Taifa ya Argentina na nje ya uwanja akaendelea kufunga magoli kama kawa na akawa akibadilisha milupo kutoka mataifa mbalimbali. 

Kutokana na hulka hiyo ya kupenda ngono, SERGIO alipoulizwa na Jack Milmall, mwandishi wa "The Mirror", ni kwanini anapenda sana vidosho, alijibu kuwa akifanya ngono siku moja kabla ya mechi, kesho yake anakuwa kwenye kuwango bora kabisa na huwa na utulivu wa aina yake alikaribiapo goli!.

Hata hivyo kama inavyowatokeaga watu wengi wapenda Totoz kwamba fedheha huwa haichezi nao mbali, SERGIO alipata fedheha kubwa tarehe 28 Septemba 2017, siku mbili kabla ya mechi ngumu ya ligi dhidi ya CHELSEA.

SERGIO alikuwa amekwea pipa na kwenda jiji la maraha la Amsterdam ambako alikwenda Pub maarufu ya mabilionea jijini humo, Cancula Pub, ambako alijirusha na vimwana hadi usiku wa manani.

Ilipofika saa 8.30, SERGIO aliondoka na vishtobe watano na kwa gari jeusi kwenda nao hotelini kwake. Hata hivyo, kutokana na kuwa alikuwa "bwaksi" kwani alikuwa "amepiga vyombo" kisawasawa, SERGIO aliuvaa mstimu na kuvunjika mbavu mbili huku kidosho GRACE JUDAKGIK akichanika sikio na mwingine JANE PINKPALL akivunjika bega!.

Kuna kila aina ya dalili kuwa BEN atarithi si tu kipaji cha soka toka kwa baba yake, SERGIO AGUERO, bali pia mambo ya kupenda vimwana. Hii ni kwasababu mara kwa mara BEN huonekana akifurahia kukumbatiwa na vitoto visichana ambavyo wazazi wao huenda navyo kushuhudia mechi kwenye Academy ya Man City ambako BEN daima hutakata vilivyo!.

Aidha, BEN anatarajiwa kurithi si tu kipaji cha mpira bali pia cha kupenda mademu toka kwa babu yake, DIEGO MARADONA. MARADONA amezaa na michepuko nane watoto nane nchini Italy, Agentina na Cuba akiwemo GIANNINA! Tarehe 8 Machi 2019, MARADONA aliumbuka na alilazimika kuwakubali watoto watatu baada ya DNA kumuumbua kwa watoto aliozaa na michepuko mitatu tofauti ya Cuba ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matumizi ya ngada toka 2000 hadi 2005!.

5. BEN Amkubali KYLIAN MBAPPE:

Ungetazamia mtoto wa magwiji hao wa kabumbu angemtaja mmoja wapo kati ya MARADONA, AGUERO au MESSI kuwa ndiye 'Idol" wake lakini BEN amewashangaza wengi kwa kusema ye hawamaindi wote hao ila anamuhusudu sana Mnyama KYLIAN MBAPPE!!.

KILA LA KHERI DOGO BEN "KUN" AGUERO!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...