Benki ya Azania (ABL) imefungua maduka matano maalum kwa ajili ya kubadirishia fedha za kigeni katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Kilimanjaro ili kuwapa fursa wateja wa benki hiyo pamoja na wananchi wote njia rahisi ya kuweza kupata huduma hiyo muhimu katika sekta ya kifedha nchini Tanzania.

Maduka ya kubadirishia fedha yaliyofunguliwa ni pamoja na katika Jengo la IPS na Hoteli ya Seacliff jijini Dar es Salaam. Maduka mengine yamefunguliwa jijini Arusha, KIA pamoja na Moshi. Huduma za kubadirishia fedha za kigeni zitakuwa zikitolewa kwenye maduka hayo kwa saa za kawaida za kazi kama matawi mengine ya Benki ya Azania.

Uamuzi wa kufungua maduka haya mapya maalum kwa ajili ya huduma za kubadirishia fedha za kigeni tu, unatokana na mwongozo wa hivi karibuni wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kama hatua ya kuhakikisha watoa huduma wote wa kubadiri fedha za kigeni wanatambuliwa na BoT.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa Benki ya Azania kufungua maduka hayo mapya, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Charles J Itembe amesema benki inajivunia kupanua wigo wake hususani katika kutoa huduma za kubadirisha fedha za kigeni katika maeneo mbalimbali nchini hasa katika maeneo yenye uhitaji mkubwa zaidi wa huduma hiyo.

“Licha ya kutoa huduma ya kubadiri fedha za kigeni, maduka haya mapya yatakuwa na uwezo wa kutoa huduma nyingine za kibenki kama vile kufungua akaunti, kuweka na kutoa fedha pamoja na huduma za kifedha kwenye simu za mkononi (sim banking)”. Amesema Itembe.

Itembe pia ameongeza kuwa Benki ya Azania itaendelea kuwa na madirisha ya kubadiri fedha za kigeni kwenye matawi yake yote nchini mbayo huwa wazi kila siku kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...