Meneja wa benki ya posta Tanzania tawi la Tunduru Bi Emajackline Mtemba akiongea na wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi, wazazi na walimu wakati alipokuwa akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru iliyofanyika katika ukumbi wa klasta Mlingoti. 
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi akimvisha kofia ya kujikinga na mionzi ya jua (pama) wakati alipokua akipokea vifaa kutoka kwa meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba vyenye thamani Tsh 2949,000.00 katika halfa iliyofanyika ukumbu wa klasta. 
Katika picha ni viongozi wa Benki ya Posta Tawi la Tunduru, viongozi wa Idara ya Elimu Msingi na watoto wenye Ulemavu wa ngozi baada ya kukabidhiwa vifaa saidi kwa ajili ya kujikinga na madhara yatokanayo na jua na magonjwa ya ngozi. 
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Gasper Zahoro Balyomi akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru vilivyotolewa na benki ya Posta tawi la Tunduru. 
******************************** 



Benki ya posta Tanzania Tawi la Tunduru imekabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 2,949,000.00 kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi vyenye wa ngozi waliopo katika shule za msingi na sekondari wilayani Tunduru. 

Akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru Ndg Gasper Balyomi Meneja wa Benki ya Posta tawi la Tunduru Bi.Emajackline Mtemba alisema vifaa hivyo ni mafuta kinga, kofia za kujikinga na mionzi ya jua (pama), Miwani, Sabuni za kuoga, na Viookuza (Magnifier). 

Bi Mtemba aliwaasa watoto hao kutumia vifaa hivyo kusoma vizuri na view chachu ya kuongeza bidii katika masomo yao,kuweni na nidhamu kwa kutii wazazi na walimu “lakini vifaa hivi viwe chachu kwenu ya kusoma na kufanya vizuri Zaidi kwenye masomo yenu kwani nyie ndio viongozi wa baadaye na ni matarajio ya benki ya posta ya Tanzania kuwa watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi wana nafasi kwenye jamii kama walivyo watoto wengine na ndio viongozi wa baadaye”

Nitoe wito kwa wazazi wote kuacha tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu wa ngozi kwani wao wana haki ya kupata elimu kwani ni haki ya msingi kwa kila mtoto na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inawatambua na kuwajali, pia niwakumbushe wazazi kuwawekea watoto Amana kwa ajili ya kusomea ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa Ada. 

Akitoa taarifa fupi ya Halmashauri ya Tunduru mgeni rasmi ambaye pia
Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Gasper Zahaoro Balyomi alianza kwa kuishukuru benki ya posta Tanzania tawi la Tunduru kutoa vifaa saidizi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wilayani Tunduru ambapo alipokea kofia 72, mafuta kinga chupa 72,sabuni 72, miwani na viookuza kwa ajili ya kugawa kwa wanafunzi hao.

Gasper Balyomi aliendelea kusema Halmashauri ya Tunduru ina shule 149 za
serikali kati ya hizo ndio zilizo na vitengo vya elimu maalum, ambazo ni Tunduru Mchanganyiko na Namiungo shule ya Msingi. 

“Tunduru ina shule za msingi 149 za serikali na shule mbili za Namiungo na
Tunduru Mchanganyiko ndio wanapokea watoto wenye mahitaji maalum, lakini ina idadi ya wanafunzi wenye ulemavu 432 ikiwa wasichana ni 167 na wavulana 265, na upande wa shule za sekondari ina wanafunzi 27, wasichana 12 na wavulana 15, lakini watoto wenye ulemavu wa ngozi ni 36 ikiwa wasichana ni 19 na wavulana 17”alisema Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Tunduru. 

Aidha alisema changamoto kubwa wanayokumbana nayo watoto hawa wenye ulemavu wa ngozi ni pamoja na kukosekana kwa mafuta kinga, miwani, kofia za kujikinga na mionzi ya jua (Pama), lakini pia kukosekana kwa huduma za matitabu ya ngozi katika hospitali za wilaya na badala yake zinapatikana katika hospitali zenye vitengo maalumu kama hospitali KCMC iliyopo Moshi, Bugando mwanza na Muhimbili ambapo wazazi wanashindwa kumudu gharama za kuwasafirisha watoto hawa. 

Aliendelea kutanabaisha kwa kusema Halmashauri ina walemavu wa aina
mbalimbali hivyo ni vyema jamii na wadau wa maendeleo kujitokeza katika
kuwawesha ili waweze kusoma na kufikia malengo yao kwani miongoni mwa 

hawa watoto wapo wenye vipaji ambavyo vinahitaji kuendelezwa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa Halmashauri ina mpango mkakati wa kuanzisha ya shule ya watoto wenye mahitaji maalum kwa ajili ya wanafunzi wa sekondari ambao wakifaulu wanashindwa kuendelea na masomo. 

Sambamba na kuanzishwa kwa shule hiyo lakini kwa sasa tuna mikakati ya
kuiombea shule ya sekondari Nandembo iliyopo wilayani Tunduru mkoa wa
Ruvuma kuanzisha kitengo cha Elimu maalum ili kupunguza changamoto ya
wanafunzi wanaofaulu kuendelea na masomo ya juu kutumia nafasi zao kwani wengi wanashindwa kwenda shule wanazopangiwa nje ya wilaya kutokana na wazazi kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama. 

Akitoa shukrani kwa niaba ya Halmshauri ya Tunduru Kaimu afisa elimu Bi Loya Mwajabu kwa Benki ya Posta Tawi la Tunduru alisema serikali kupitia sera ya elimu ya mwaka 2004 haijabagua watoto kwani watoto wote ni sawa na wanatakiwa kupata elimu kwani ni haki ya msingi. 

Alisema Kupata elimu kwa watoto kutamsaidia mtoto kujitambua na kupata urithi ulio sahihi, mama ni mlezi mkubwa na nikuhakikishie kuwa hawa watoto watatumia vifaa hivi vile iliyoelekezwa, wito wetu kwa jamii ni kuwa hawa wamezaliwa hivi walivyo na wana haki ya kupata elimu kwani ndio ukombozi wao. 

Aidha niwaombe wazazi, jamii na wadau wa elimu na maendeleo ndani nan je ya wilaya ya Tunduru kuguswa na watoto hawa, kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia vifaa saidizi watoto kwani watoto 432 wenye ulemavu ni wengi sana na sio hawa wenye ulemavu wa ngozi tuu,pia wapo wenye mtindio wa ubongo, bubu viziwi, viwete na wote hawa wanahitaji kusaidiwa kufikia ndoto zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...