Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akipokea zawadi ya picha kutoka kwa moja wa wafanyabiashara wa madini 
Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha lililozinduliwa rasmi jana.
Baadhi ya wafanyabiashara wa vito vya madini wakifatilia kwa makini 
waziri Biteko akiangalia baadhi ya vito vilivyopo katika soko hilo
baadhi ya wafanyabiashara wakiangalia vito vilivyopo katika soko hilo 
Mwenyekiti wa TAMIDA, Sammy Mollel akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alishukuru kwa kuanzishwa kwa soko la madini pia alipongeza serikali kwa bajeti ya mwaka 2019/20 kwani imeondoa kilio cha muda mrefu cha wachimbaji na wauzaji wa madini nchini.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea katika uzinduzi huo
Mbunge wa viti maalumu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya bunge nishati na madini Catherine Magige akiongea katika uzinduzi huo 


Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Waziri wa madini Doto Mashaka Biteko,amewataka wafanyabishara wa madini wadogo pamoja na wakubwa kuwafichua wafanyabiashara wote wanaojaribu kutorosha madini pamoja na wale ambao wanaokwepa kulipa kodi ya serikali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao

Hayo ameyasema leo wakati wa uzinduzi wa soko la madini mkoani Arusha ,ambapo alisema kuwa Iwapo wafanya biashara watakuwa wawazi na watafichua watu wote ambao wanakwepa kodi na kutorosha madini hitasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi yetu.

Alisema kuwa ili kuweza kuinua uchumi wan chi yetu ni lazima kila mwananchi kutimiza wajibu wake kwa kulipa kodi kwa uaminifu ili kusaidia kukuza uchumi wan chi yetu aidha alisisitiza kuwa heshima kubwa ya mtanzania ni kulipa kodi na sio kufanya mambo ya kijanja janja na alibainisha kuwa ni lazima watanzania tuhame katika taifa la watu wajanja wajanja tuwe wananchi wa taifa la watu waaminifu .

“mlilalamika kuhusiana na kodi tumefanyia kazi na yale ambayo bado tutafanyia kazi lakini kwa kuwa tumefanyia kazi na nyie rudisheni fadhila kwa kulipa kodi ,na pia napenda kuwasihi wenyeviti wa mabroka kuwakusanya mabroka ambao hawajalipa kodi kulipa kodi wakate leseni ili nao wawe katika orodha ya walipa kodi”alisema Biteko

Alibainisha kuwa, tangu kuingia madarakani kwa Serikali ya Awamu ya Tano, imekuwa ikisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha Sekta ya Madini inakua, inanufaisha watanzania pamoja na kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.Aliendelea kueleza kuwa Serikali pia imefuta baadhi ya tozo ambazo zilikuwa kero kwa wafanyabiashara wa madini hususani wachimbaji wadogo na kufafanua kuwa tozo hizo kuwa ni pamoja na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) asilimia 18 na kodi ya zuio ya asilimia tano kwa wachimbaji wadogo.

Alibainisha kuwa kuwekwa kwa soko hili hapa Arusha kunasaida kuwepo kwa mazingira mazuri ya kibiashara kwenye sekta ya madini pamoja na kufuta kodi na tozo mbalimbali zinazofikia asilimia 23 na pia soko hili litasaidia kuondoa utoroshwaji wa madini na kusaidia wachimbaji wadogo kutambuliwa.

Alieleza manufaa mengine kuwa ni pamoja na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za wachimbaji wadogo na kuongeza wigo wa mapato ya nchi.“napenda kuwasihi wachimbaji wote wadogo na wafanyabiashara wa madini kuendelea kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali katika kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali” alisema Biteko .

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa manufaa ya soko jipya la madini litasaidia kuziba mianya ambayo imekuwa chanzo cha utoroshwaji wa madini, ukwepaji kodi na hivyo kusababisha biashara nzima ya madini kufanyika kiholela katika maeneo mengi ya nchi.

Aliongeza kuwa soko hili litasaidia kuwezesha na kurahisisha biashara nzima ya madini na kuwa kiungo muhimu cha kuwakutanisha wachimbaji na wafanyabiashara kwa lengo la kuuza na kununua madini.aliendelea kufafanua manufaa mengine ya soko kuwa ni pamoja na kuwa suluhisho la tatizo la kupunjwa na kudhulumiwa na kuondoa vitendo vya dhuluma ambavyo vimekuwa vikiwahusisha wafanyabiashara wa madini wasiokuwa waaminifu kwa baadhi ya wachimbaji wadogo.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoani Arusha ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu Bunge nishati na madini Catherine Magige alisema kuwa Soko hili litaondoa uwezekano wa wanunuzi wa madini kuibiwa na wajanja wachache wanaojifanya kuwa na madini wakati hawana.Alitumia mda huo kuwasihi wanunuzi wa madini kulitumia soko kikamilifu ili kuepuka udanganyifu na matapeli tu
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gamboa akiongea katika uzinduzi wa kituo cha uuzaji madini mkoa hapa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...