Boomplay, app inayoongoza barani Afrika kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki, yafanya forum yake ya kwanza kwa ajili ya wasanii nchini Tanzania. 

Katika forum hiyo, Meneja wa Boomplay Tanzania Bi Natasha Stambuli alizungumza kuhusu kuwezesha wasanii na uzalishaji wa muziki (Production) na usambazaji wa muziki kidigitali (Digital Distribution).

“Boomplay tunatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii kama kupata muda wa studio, ku-shoot video zenye quality ya kimataifa na mengine mengi. Tumeingia mkataba na Wanene Entertainment ili kuwezesha wasanii na matatizo hayo.”

“Barani Afrika Boomplay ina ofisi Tanzania pamoja na Kenya, Nigeria na Ghana. Moja kati ya fursa zinazopatikana ni sisi kuwa na uwezo wa kujenga madaraja kwa wasanii wetu wa Tanzania na wasanii wengine kutoka nchi hizo” aliendelea Bi Natasha Stambuli.

Forum hiyo ilijumuisha jopo la wataalamu mbalimbali katika tasnia ya muziki akiwemo Bi Martha Huro - Meneja wa Boomplay Kenya, Lupakisyo Mwambinga - Mkuu wa Idara Ya Sheria COSOTA, Nahreel kutoka Navy Kenzo, Moses Range - Muanzilishi DEMO Innovators, Japhet Kapinga - Meneja Maudhui Boomplay na kuratibiwa na msanii wa miondoko ya Hip Hop, Wakazi.

Wasanii na watayarishaji pia walipata nafasi ya kuuliza maswali kwa wataalamu hao na kupata ujuzi zaidi katika masuala ya sheria, hati miliki, branding na vingine vingi katika tasnia ya muziki. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...