MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo wilayani imefanyika katika Kijiji cha Kimbo kata ya Potwe Tarafa ya Bwembwera. 
Mkurugenzi wa Mazingira Wizara Maji Obadia Kibona akizungumza wakati wa maadhimisho 
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akipanda miti kwenye maadhimisho hayo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio hayo
MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanaasha Tumbo amewataka wazazi na na walimu kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mti mmoja shule na nyumbani ikiwa ni kampeni endelevu ya uhifadhiwa wa mazingira 

Amesema kuwa utekelezaji wa agizo hilo utaweza kuendesha kampeni endelevu ya uhifadhi wa Mazingira na vyanzo vya maji jambo ambalo litasaidia uwepo wa miti ya kutosha kwenye maeneo yenye vyanzo hivyo 

Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Mazingira Duniani ambayo wilayani imefanyika katika Kijiji cha Kimbo kata ya Potwe Tarafa ya Bwembwera. 

Katika maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji,Bonde la Maji la Mto Pangani,Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira( Tanga Uwasa),Umoja wa Utaunzaji Mazingira na Vyanzo vya Maji mto Zigi(Uwamakizi)na viongozi wengine wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza. 

Amesema kuwa katika kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri na rafiki kila mwanafunzi anatakiwa kupanda miti miwili mmoja nyumbani na mwingine shule. " Natoa agizo kwa wazazi na walimu kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa amepanda mti mmoja nyumbani na mwingine shule ili tuweze kuyatunza mazingira na vyanzo vya maji" alisema. 

Aidha alisema mbali na hilo pia kuwe na utaratibu wa kila siku watoto wajengewe utaratibu wa kuokota takataka za mufuko ya plastiki inayozagaa ovyo. Awali akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa m Jumuiya ya Watumia Maji zigi juu Philipo Mdoe alisema baadhi ya wavuvi waliopo kwenye vijiji sita vilivyopo kata mbalimbali wilayani humo wanadaiwa kuvua kwa kutumia sumu za mimea na viwandani kwa ajili ya kuua samaki. 

Alisema kwamba hatua hiyo imeanza kuleta hofu kubwa kwa watumiaji wa maji ya Mto Zigi ambao hutumiwa na wakazi zaidi ya 600,000 waliopo wilayani humo na Jiji la Tanga. 

Aidha alisema uchunguzi walioufanya katika vijiji hivyo wamebaini kuwa sumu inayomwagwa kwa ajili ya kuua samaki ni ile ya mimea inayojulikana kwa jina la Deles ileya viwandani aina ya DIP inayotumika kuogeshea wanyama. 

Akielezea udhibiti wanaoufanya kudhibiti vitendo hivyo,Mjumbe wa Kamati ya Mazingira Zigi Juu Awadhi Shauri alisema wavuvi hao hufanya kazi hiyo nyakati za usiku kuanzia saa nane mpaka saa tisa hivyo wanaiomba serikali na mamlaka husika kutoa msaada wa kwa sababu kamati za mazingira zilizoundwa hazikidhi mahitaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...