Rais Mstaafu wa awamu nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete


Na Bakari Madjeshi wa Michuzi TV

Rais Mstaafu wa awamu nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa katika mchezo wa Soka ukiwa Kiongozi kwa madaraka yeyote ya Serikali kila timu inakuhusu. 

Akizungumza katika harambee ya hamasa yakuichangia timu ya Yanga SC ijulikanayo kama 'KUBWA KULIKO', Dkt Kikwete amesema utakuwa Kiongozi mwenye dhamana mpuuzi kukandamiza timu nyingine kwa madaraka yako.

"Kuna Wakati mtu kama Juma Kapuya alikuwa Kiongzi katika Serikali lakini alikuwa Simba kindakindaki hawakutumia nafasi ile kukandamiza timu ya Yanga basi kama angefanya hivyo ingebidi tutafute Waziri mwengine ashughulike na Yanga SC ", amesema Dkt Kikwete.

Katika shughuli hiyo pia, Dkt. Kikwete ameuliza: "Waziri Mkuu sijui timu yako?lakini umekubali mwaliko huu, umefanya jambo la maana sana, tushukuru suala hili, tumpomgeze sana, tusitumie nafasi hii kupiga vijembe Viongozi, ngonjeni watoke madarakani".

KUHUSU SUALA LA KLABU YA SIMBA KUJENGA UWANJA WA BUNJU


Dkt. kikwete amesema kuwa Klabu ya Simba walipokuwa wanataka kujenga Uwanja wa Mabwepande amedai walihitaji kiasi cha pesa Shilingi Milioni 30 ambapo timu hiyo ilimtumtumia Rais wa Klabu hiyo wakati huo, Ismail aden Rage kuomba pesa hizo.

"Na kweli Simba SC walipata uwanja kipindi hicho, na mimi nasema hayo kukumbushia kuwa huu ni wajibu wa Viongozi", amesema Dkt. kikwete.

Hata hivyo, Dkt. Kikwete amemuomba Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa kuichangia Yanga SC kwa kutoa chochote, pamoja nakumfikishia ujumbe Rais Dkt. John Pombe Magufuli na yeye kuchangia Yanga SC.

"Nilichangia Simba kupata Milioni 30 Simba Wakapata Uwanja, sisemi mrudishe zile hela ila nawaombea Yanga mchango kutoka kwenu," alieleza Dkt. Kikwete.

Pia amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu zote kuwa na hisia za timu zao sambamba na pale zinapokuwa uwanjani zinacheza, amesema kuwa huwa hapendi kwenda uwanjani lakini amesema Simba wanachangamka,  Yanga SC hawachangamki kama Simba SC.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kikwete amewataka Yanga SC kuwa na Mipango, Mifumo yakuendesha Klabu hiyo kisasa pamoja nakuwekeza katika Soka la Vijana.


Dkt. Kikwete ametolea mfano Kocha wa zamani wa Yanga SC kutoka Romania, Victor Stanslaus kuwa aliwekeza zaidi katika Soka la Vijana ambapo vipaji kadhaa vilizaliwa mfano kina Sunday Manara, Mohammed Rishard, Kassim Manara.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa na Uchangishaji ya Yanga,Anthony Mavunde akizungumza na vingozi mbalimbali na mashabiki wa tumi ya Yanga leo wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO katika Ukumbi wa Diamond Jubilee. (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa wakati alipowasili katika ukumbi wa Diamond Jubilee.





 Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanzana kulia) akiteta jambo na viongozi mbalimbali wakati wa hafla ya KUBWA KULIKO katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo jijini Dar es Salaam.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...