Na Mwandishi wetu Mihambwe 

Afisa Tarafa Mihambwe Emmanuel Shilatu Leo Jumamosi Juni 15, 2019 ameshiriki zoezi la usafi wa mazingira akishirikiana na viongozi pamoja na Wananchi wa kata ya Kitama. 

Gavana Shilatu aliwasihi Wananchi wote kuhakikisha wanasafisha na kuyatunza mazingira ili nayo yawatunze ikiwemo kila iitwapo jumamosi kuwa ni siku ya usafi wa mazingira. 

*”Nimetoa maelekezo kwa Watendaji kata na Vijiji kuhakikisha kila iitwapo jumamosi ndani ya Tarafa ya Mihambwe wanashiriki na kusimamia zoezi la kitaifa la usafi wa mazingira na wakati wote wanahakikisha maeneo yao ni safi. Nami nimekuja hapa kuonyesha kwa vitendo kwamba suala la usafi wa mazingira ni jukumu letu sote.”* Alisema Gavana Shilatu. 

Usafi wa mazingira wa kila jumamosi ni agizo na kampeni ya kitaifa ambayo kila Mtu anapaswa kuitii kwa kufanya usafi na kuyatunza mazingira yawe safi nyakati zote. 

Katika zoezi hilo la usafi wa mazingira Gavana Shilatu aliambata na Watendaji kata na Vijiji wakishirikiana na Serikali za Vijiji pamoja na Wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...