* Yawakutanisha wajasiriamali, wanafunzi na wafanyabiashara na kuwajengea ujuzi kuhusiana na masuala ya mauzo, masoko pamoja na teknolojia.

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
UWEZESHAJI wa kiuchumi kwa wananchi kwa kuwapa maarifa mapya na namna bora ya kufanya biashara yameelezwa kuwa ni nyenzo muhimu ya kujenga uchumi imara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya mafunzo yaliyowakutanisha wafanyabiashara, wajasiriamali, wadau na wanafunzi Mkurugenzi wa mauzo na masoko Afrika Mashariki kutoka hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam Denis Glibiv Cluster amesema semina hiyo iliyowakutanisha wanajamii na wataalamu imelenga  vitu 4 muhimu katika biashara ikiwemo mauzo, na masoko na namna bora ya kutumia teknolojia.

Ameeleza kuwa wamewaleta wataalamu kutoa nje (Dubai na Afrika Kusini) na wataalamu wa ndani ya nchi  kwa malengo ya kujenga jamii ya kibiashara na kueleza kuwa wamepata matokeo chanya kutoka kwa washiriki 70 na mkutano ujao utakaofanyika mwezi Novemba wataongeza idadi kubwa ya washiriki ili ujumbe kuhusiana na biashara na uchumi uweze kufika kwa wananchi kote nchini.

Kwa upande wake Meneja mawasiliano na masoko wa hoteli hiyo Lilian Kisasa amesema kuwa semina hiyo imefanywa kwa majadiliano na vitendo na hiyo ni baada ya kuona kuna tofauti kubwa kati ya teknolojia na wafanyabiashara hivyo wakaona ni vyema kuwaalika wadau hao ili kutoa fursa kuhusiana na maarifa ya kiuchumi.

Amesema kuwa watu wengi hawajawa na uelewa juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii ambayo kwa sasa ndio njia bora kukuza biashara na sio kwa burudani pekee na wana imani kuwa baada ya mafunzo hayo washiriki watakuwa mabalozi kwa wengine.

"Ni mkutano wa kwanza kuufanya na umelenga kuwekeza katika biashara, uchumi na teknolojia kwa wajasiriamali, wanafunzi na wafanyabiashara  na wataalamu waliotoa mafunzo hayo kwa kada mbalimbali wametoka hapa nchini na nje ya nchi na hiyo yote ni kwa malengo ya kujifunza mambo mapya kwa wakati huu wa mapinduzi ya kiteknolojia" ameeleza Lilian. 

Pia amesema kuwa  kitu cha tofauti walichoona kutoka kwa washiriki ni  kufurahia kwa kushiriki na kujifunza vitu vipya huku
 akisema kuwa watakutana tena na wadau hao mwezi Novemba mwaka huu ili kuendelea kujenga uelewa zaidi kuhusiana na biashara ukuaji wa uchumi.
 Mkurugenzi wa mauzo na masoko Afrika Mashariki kutoka hoteli ya Hyatt Regency Denis Glibic Cluster akizungunza wakati wa semina hiyo iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa biashara na uchumi pamoja na wanafunzi,  jijini Dar es Salaam.
 Washiriki mbalimbali wakisikiliza mafunzo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa semina hiyo,  jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi wa semina hiyo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...