Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, amewataka Maofisa na askari kuhakikisha wanaendelea kutimiza wajibu wao kikamilifu na kutokujiingiza kwenye masuala ya uhalifu ikiwemo kushiriki kwenye wizi wa dhahabu sambamba na uhujum uchumi.

IGP Sirro, ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa akizungumza na Maofisa na Wakaguzi wa Jeshi hilo ambapo amesema kuwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa askari anayeshiriki kwenye uhalifu ikiwemo kufukuzwa kazi pamojana kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo IGP Sirro amesema Jeshi la Polisi limejipanga kikamilifu katika kuhakikisha suala la uchaguzi linafanyika kwa amani na utulivu na kwamba amewahakikishia wananchi usalama wao na mali zao na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa sahihi za uhalifu na wahalifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...