Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(Mb) ameagiza ujenzi wa Hospital ya Uhuru uanze Wiki ijayo Tar.24/06/2019 ili kutimizia ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa Dec, 2018 na kuelekeza fedha kwa ajili ya kazi hiyo.
Waziri Jafo alitoa maagizo hayo wakati wa ziara yake Wilayani Chamwino kukagua ujenzi wa hospital hiyo ya kisasa na  kukuta  hakuna ujenzi ulioanza na hata eneo  hilo halijasafishwa.
Akizungumza katika ziara hiyo Jafo amesema hataki kusikia hadithi zozote zinazokwamisha kuanza kwa ujenzi wa Hospital ya Uhuru kwa sababu Agizo lilishatoka na fedha zilishatengwa.

“Sikutarajia kukuta eneo la ujenzi likiwa katika hali hii, hakuna kitu kilichofanyika mpaka leo halafu mnaniambia bado mnaendelea na vikao sijui mnajadili nini ambacho hakiishi ninachotaka kuona hapa ni ujenzi kuanza mara moja yaani ikifika Jumatatu hali ya hapa iwe tofauti mkamilishe mambo yote yanayotakiwa kwa siku hizi chache na kazi hii ianze”

Waziri Jafo aliongeza kuwa nimesikia bado mnajadili kuhusu ramani gani itumike katika ujenzi huu sasa naagiza ujenzi wa Hospital hii utumie ramani ya Hospital ya Tunduma ambayo ni Gorofa kwa sababu ramani ile  itasaidia katika matumizi bora ya Ardhi na pia itakidhi mahitaji ya kuwa na jengo la kisasa lenye hadhi ya Hospital ya Uhuru.

Wakati huo huo Waziri Jafo aliagiza  kikosi maalumu cha SUMA JKT kitumike katika ujenzi wa hospital ya Uhuru ili iweze kwenda na muda na  ubora uweze kuzingatiwa na Wakala wa Majengo (TBA) watumike kama washauri na wadhibiti Ubora wa Majengo ya Hospital hiyo.

“Natoa miezi sita ujenzi wa Hospital hii uwe umekamilika na  ndio maana nikaagiza Kikosi cha Jeshi SUMAJKT  kitumike  ili tuweze kwenda na muda kwahiyo ifikapo Dec, 2019 nataka kuja kuona majengo yote  ya Hospiatl yakiwa yamekamika na kwa ubora wa hali ya juu” Alisema Jafo.

Akitaja sababu zilizochelewesha ujenzi wa Hospital ya Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Belnith Mahenge amesem  michoro ya Hospital imechelewa kupatikana na zaidi fedha zilizoelekezwa hazijaingia kwenye Akaunti husika ili ziweze kutumika kwenye  ujenzi.

Aidha Rc Mahenge  alimshkuru Waziri Jafo kwa ziara yake na kusema maagizo yote yaliyotolewa yamepokelewa  na yatatekelezwa; Ujenzi wa Hospital ya Uhuru  utaanza mara moja.

Ujenzi wa Hospital ya Uhuru ni Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilolitoa mwezi Dec, 2018 ambapo aliagiza shilingi bil. 900  zilizokuwa zitumike kwenye  sherehe za maadhimisho ya Uhuru  wa Tanzania zitumike kujenga Hospital Kisasa Mkoani Dodoma na  kuongezafedha zaidi shilingi  Bil 2.5 kutoka katika Gawiwo lililotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Airtel.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo akitoa maelekezo katika eneo la ujenzi wa Hospital ya Uhuru inayojengwa katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...