Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MBUNGE wa Jimbo la Starehe nchini Kenya Charles Njagua maarufu kama Jaguar amekamatwa na polisi nchini humo kufuatia kauli yake yenye utata dhidi ya wawekezaji.

Jaguar ambaye bado anashikiliwa na polisi amekamatwa leo jumatano katika viwanja vya bunge na hiyo ni baada ya kushindwa kuripoti katika kituo cha polisi kama alivyoagizwa .

Serikali nchini Kenya imejiweka kando na kauli hiyo ya Jaguar ambayo ilipinga kufanya biashara na na wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nchi za nje.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka ilikemea Uhuru wa kuongea uluotumiwa na mbunge huyo katika kudhalilisha wawekezaji kitu ambacho si utamaduni wa nchi hiyo na unapaswa kukemewa.

Kupitia video iliyosambaa kupitia mitandao ya kijamii Jaguar alionekana akikemea uwepo wa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka nje na kueleza kuwa wataondolewa kwa nguvu wasipotii agizo Hilo.

Lakini Waziri wa mambo ya nje Macharia Kamau amesema kuwa Kenya imesikitishwa Sana na kauli ya Mbunge huyo hukuakieleza kuwa serikali ya Kenya haikubaliani na kauli hiyo na amewahakikishia usalama kwa wawekezaji wote nchini humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CCM daima kwani sera zake na ilani yake zinatekelezeka. Kidumu chama cha mapinduzi...kidumu chama tawala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...