JESHI la Magereza limekabidhi cheti maalum cha kuishukuru Benki ya NMB kwa msaada wa fulana ambao iliutoa kwa wanamichezo walioshiriki tamasha la michezo kati ya Magereza Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.

Cheti hicho maalum kimekabidhiwa leo na Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa kwa Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite ikiwa ni kutambua mchango wa benki hiyo mara kwa mara.

Akizungumza kwa niaba ya Jeshi la Magereza kabla ya kukabidhi cheti hicho, afisa huyo alisema wataendelea kujenga ushirikiano mzuri na benki hiyo kwa kuwa inawathamini hata maeneo mengine ya kijamii.

Kwa upande wake Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite alilishukuru Jeshi la Magereza kwa kutambua mchango na mahusiano mazuri kati ya pande hizo na kusema NMB itaendeleza ushirikiano huo. Aliongeza kwa sasa Benki hiyo imekuja na bidhaa bora zaidi ambazo wateja wao hasa taasisi zinazofanya biashara nao itafurahiya bidhaa hizo.
 Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kulia) kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kulia ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB wakishuhudia tukio hilo.

 Maofisa washiriki katika tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo fupi.
 Ofisa Michezo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Matilda Mlawa (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti maalum cha shukrani Meneja Mwandamizi Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ally Ngingite kwa kutambua mchango wa benki hiyo ambao imekuwa ikiutoa kwa wanamichezo wa Magereza. Wa kwanza kushoto ni Ofisa Michezo Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Mrakibu waMagereza, Joseph Siwale pamoja na maofisa wa NMB (kulia) wakishuhudia tukio hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...