Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imesema kuwa inadai kiasi cha fedha cha shilingi Bilioni 4 kama tozo za umwagaji wa taka katika dampo la Pugu jijini Dar es Salaam.

Deni hilo limeeelezwa leo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji kilichofanyika katika ukumbi wa karimjee jijini Dar es Salaam.

Akitoa ufafanuzi huo Mstahiki Meya wa, Isaya Mwita Amesema kuwa Jiji limekuwa likitoa huduma ya utupaji taka katika dampo la kinyamwezi lakini Halmashauri zote zimeshindwa kulipa Deni hilo hadi likafika shilingi Bilioni 4.

"Fedha hizi ni za umma na ndio chanzo cha mapato ya jiji hivyo tunaomba mameya waweze kuwambia wakurugenzi wao kuwa walipe fedha hiyo hili ripoti ya CAG yetu iwe safi" amesema Mwita.

Kwa upande wake Meya wa Ubungo, Boniface Jacob ameeleza kuwa deni hilo halipo  kwani wao Kama Halmashauri wanalidai jiji zaidi ya shilingi Bilioni 5 hivyo kusema wanadaiwa shilingi bilioni nne si sahihi.

Meya Jacob amesema kuwa  jambo lilipo ni kukaa chini na kuwekeana makubaliano ili waweze kufikia muafaka.

Hata hivyo hoja zingine zilizoibuka katika Baraza Hilo ni uhalali wa umiliki wa soko la kariakoo kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Baraza hilo limeazimia Kamati ya fedha ya jiji  kukaa tena na kujadili ili waweze kujua ni njia gani zitatumika kwa jiji hilo ili   liweze kupata hati ya umiliki wa hisa za soko la kariakoo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana alisema kinachotakiwa kufanyika ni makubaliano ya mawaziri wa pande Mbili zinazo miliki soko hilo na kueleza kuwa Kama Waziri wa Tamisemi na Waziri wa fedha wakikaa  na kujadili hoja hiyo basi mafikiano yatakuwa rahisi na kila uapande utapata haki yake na kupewa gawio la mapato la kila mwaka.
 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijii Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana akitoa ufafanuzi kuhusu hoja zilizowasilishwa na mkaguzi was hesabu za serikali kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijii Dar es Salaam.
 Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob akizungumza juu ya hisa za Halmashauri katika kiwanda Cha nyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijii Dar es Salaam
 Diwani wa Mwananyamala ,Songoro Mnyonge akitetea hoja ya Halmashauri kupatiwa hisa katika kiwanda cha nyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijii Dar es Salaam
 Diwani Viti Maalum Kata ya Kigamboni,Amina Yakub akisistiza Jambo wakati was kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijii Dar es Salaam.
 Mbunge wa Kawe Halima Mdee akichangia mada katika kikao cha Baraza la Madiwani la jiji la Dar es Salaam kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...