Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru msanii wa filamu nchini na Wema Sepetu kukaa gerezani kwa siku nane wakati akisubiri maamuzi ya dhamana.

Wema ambaye ni Miss Tanzanua 2006 ameingia matatani baada ya kutofika mahakamani hapo mara mbili bila ya sababu na mahakama kutoa hati ya kumkamata kwa kuruka dhamana.

Akitoa maamuzi hayo leo Juni 17.2019 Hakimu Mkazi, Maira Kasonde amesema kwa sababu masuala yaliyoletwa mahakamani hapo yanahusu dhamana, atatoa uamuzi Juni 24, mwaka huu kuhusiana na dhamana ya mshitakiwa 

Akijitetea kwanini asifutiwe dhamana, Wema amedai ni kweli hakufika mahakamani Mei 11 na Juni 14, mwaka huu, na kudai mara ya kwanza alisafiri kikazi nje ya mkoa ambapo alikwenda mkoani Morogoro na kwamba alimpa taarifa wakili wake na mara ya pili, alifika mahakamani lakini alishindwa kuingia kwenye chumba cha mahakama kusikiliza kesi yake kwa sababu aliumwa ghafla tumbo la hedhi.

Ameeleza kuwa, inapofika tarehe ya hedhi mara nyingi tumbo humuuma hivyo alienda hospitali kwa ajili ya kuchomwa sindano ya diclopa. Hata hivyo, aliomba mahakama imsamehe kwa kutokuhudhuria mahakamani.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda alidai mahakamani hapo kuwa, mshitakiwa hana rekodi yakutohudhuria mahakamani hivyo aliomba apewe onyo na kueleza kuwa, endapo mshitakiwa atapata udhuru ni vema kuwapa taarifa wadhamini wake ili kuepuka usumbufu kwa mahakama.

Juni 11, mwaka huu upande wa mashitaka ukiongozwa na Wakili Sylvia Mitanto ulidai mshitakiwa hayuko mahakamani na hakuna taarifa yoyote na hivyo mahakama ikatoa amri ya kukamatwa kwa mshitakiwa huyo baada ya kuruka dhamana.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani ambapo anadaiwa kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.
 ALIYEKUWA Miss Tanzania 2006  na Msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu akipanda basi la magereza tayari kwa kwenda kuishi huko hadi Juni 24.2019  wakati akisubiri maamuzi ya dhamana, baada ya kukiuka masharti.

ALIYEKUWA Miss Tanzania 2006  na Msanii wa Bongo Movie Wema Sepetu akipanda basibla magereza tayari kwa kwenda kuishi huko hadi Juni 24.2019  wakati akisubiri maamuzi ya dhamana, baada ya kukiuka masharti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...