Na Karama Kenyunko, Blobu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa sababu upande wa mashitaka umekosa kibali cha kuita mashahidi kutoka mkoani Kigoma.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga  amebainisha hayo leo Juni 17, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokija kwa kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa.

Kesi hiyo leo ilipaswa kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa shahidi wa tano wa upande wa mashtaka, wakili Katuga akadai, shauri hilo lilipangwa kusikilizwa na walishaanza utaratibu wa kupata mashahidi kutokea mkoani Kigoma lakini wamekosa kibali kutoka kwa Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu.

Kufuatia hivyo, Wakili Katuga ameiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo wakati wakifatilia kibali hicho ili wawapate mashahidi hao ambao ni takribani sita kutokea mkoani Kigoma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 16 na 17, 2019.

Katika kesi ya msingi, Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi anadaiwa kutenda makosa hayo, Oktoba 28, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama cha ACT Wazalendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...