Na woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha 

SERIKALI imewataka majangili wote popote walipo wajisalimishe vinginevyo serikali   itawatumia polisi wa kimataifa kuwakamatwa mmoja mmoja ili kutokomeza vitendo vyote vya ujangili ndani ya hifadhi zote hapa nchini.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamisi Kingwangala, alipokuwa akifungua mkutano wa kimataifa wa Utalii unaoshirikisha mataifa mbalimbali pamoja na mashirika ya kimataifa yanayohusiana na maswala ya utalii, ulimwenguni na wadau.

 Kigwangala, amesema  kuwa  katika kipindi cha miaka michache kiwango cha Ujangili wa Wanyamapori kwenye hifadhi mbalimbali nchini kimeshuka lakini biashara ya nyara  haramu inaongezeka..

Amesema  wanaouza au kusafirisha nyara ni wale waliokuwa na akiba za nyara kwani hakuna nyara mpya, na wanazisafirisha nje ya nchi na usafirisahaji wa nyara uumeipiku biashara ya usafirishaji wa binadamu ambapo biashara hiyo ya nyara imepanda hadi kushika nafasi ya tatu ya biashara haramu.

Amebainisha kuwa Mkutano huo unaangalia namna ya  kupata taarifa za ujangili  kwenye hifadhi kuangalia  namna ya kufanya kazi ,kushirikiana kupeana  taarifa kutatua migogoro inayojitokeza kati ya wananchi wanaoishi kwa kupakana na hifadhi kwenye maeneo ambako ni mapito ya wanyama pori, kuimarisha miundo mbinu  katika swala zima la kudhibiti ujangili ndani ya hifadhi mbalimbali.

Waziri Kigwangala,amesema  Usalama wa Dunia unategemea usalama wa mazingira Matokeo ya mkutano huo yatapelekwa kwenye mkutano mkuu wa marais utakaofanyika nchini Japani mwezi Augosti mwaka huu na hiyo ni fursa kwa afrika kutokomeza biashara haramu ya ujangili .

Kwa upande wake mkurugenzi msaidizi wa kuzuia ujangili  Robat Mande amesema kuwa mkutano huo inalenga kuimarisha mfumo wa Kiintelejensia ,uzoefu na nyara na mazao ya misitu.

 Amesema Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ni kinara barani Afrika katika kudhibiti vitendo vya Ujangili dhidi ya wanyama pori barani Afrika.

 Mande, ambae pia ni mwenyekiti wa kikosi cha kuzuia ujangili nchini,ameongeza kuwa ujangili huo umedhibitiwa kutokana na kutekeleza falsafa ya ushirikishawaji wa vyombo vingine vya dola pamoja na wadau na wananchi na hivyo kuwezesha kufanya kazi kwa pamoja

Amesema mwaka 2005  Tanzania ilikuwa ni moja kati ya nchi 8 Ulimwenguni ambazo ujangili ulikuwa umekithiri lakini mwaka 2014 kulizinduliwa  mkakati wa kutokomeza ujangili na sasa tupo kwenye nafasi nzuri ya kuwa ni nchi ambayo imetokomeza ujangili.

Alisema Mkutano huu ni wa tatu kufanyika mkutano wa kwanza ulifanyika Nairobi nchini Kenya nmkutano wa pili ulifanyika nchini Thailand mkutano ujao utafanyika Japani.

Nae mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka za usimamizi za wananchi ,WMA, George wambura, amesema yapo maeneo 38  ya hifadhi za wananchi kati yake 22 ndio yanayotumika  kwenye shughuli za uwindaji  na utalii na zimeweza kudhibiti ujangili kwa asilimia 88  na hivyo kuboresha utalii kwenye maeneo mbalimbali,.

Amesema zipo WMA 36,000 ambazo zimekuwa zikisaidia serikali katika kudhibiti ujangili na hivyo kuwezesha wananchi waishio kuzunguka hifadhi hizo kujipatia vipato

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...