Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Emmanuel Amunike ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye fainali za mataifa Afrika (Afcon 2019) nchini Misri.

Kikosi hicho kimetangazwa rasmi jana na Kocha Amunike kimewaacha nyota kadhaa wanaochezw soka la kulipwa nje ya nchi.

Wachezaji walioachwa ni pamoja na Beki Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Shiza Kichuya wa ENNPI ya Misri na Shaaban Iddi Chilunda wa Tenerife ya Hispania.

Wengine ni magolikipa Suleiman Salula wa Malindi SC ya Zanzibar na Claryo Boniface wa u20, David Mwantika wa Azam, Freddy Tangalu na Miraj Athumani wa Lipuli na kinda wa Serengeti Boys (U17), Kelvin John ‘Mbappe’.

Akitangaza kikosi kamili cha mwisho cha  wachezaji 23  wa Taifa Stars kwa ajili ya AFCON, Amunike amewataja ni   makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC) na Aaron Kalambo (Tanzania Prisons).

Mabeki ni Hassan Kessy (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Mohamed Hussein, Erasto Nyoni (Simba SC), Kelvin Yondan, Gardiel Michael (Yanga SC), Ally Mtoni Sonso (Lipuli FC) na Aggrey Morris (Azam FC).

Kwa upande wa safu ya Kiungo ni Feisal Salum (Yanga SC), Himid Mao (Petrojet, Misri), Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco) na Farid Mussa (Tenerife, Hispania).

Safu ya ushambuliaji ni Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Adi Yussuf (Blackpool, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, Algeria) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).

Kikosi hicho kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri utakaopigwa kesho katika Jiji la Alexandria na baadae kucheza na Zimbabwe kabla ya kuanza kwa michuano ya AFCON.

Taifa Stars wapo kundi C na Timu ya Senegal, Algeria na Kenya na mchezo wa kwanza utakuwa dhidi ya Senegal.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...