NA MWAMVUA MWINYI,MKURANGA

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, ametoa rai kwa wakandarasi katika wilaya mbalimbali kuongeza kasi ili kuhakikisha wananchi wanapata nishati vijijini ,kama ilivyo maagizo ya Rais Dk.John Magufuli mpaka 2021 vijiji vyote kuunganishiwa umeme .

Aidha ametoa rai kwa wanyakazi wa TANESCO katika Ofisi za Wilaya nchi nzima, hususan kada ya maofisa uhusiano na huduma kwa wateja, kufanya kazi kwa kujituma kwa kutoka maofisini kwenda kutafuta wateja ili kuliongezea shirika mapato.

Alisema hayo wakati akiwasha rasmi umeme kijijini hapo kwenye duka la Abdul Abdulrahman, ikiwa ni ishara ya kukiwashia kijiji kizima.Subira alieleza, mikakati ya serikali kufikisha umeme katika maeneo yote nchini.

Alisema kuwa ,matarajio ni kuvifikishia nishati hiyo vijiji 10,268 nchi nzima ifikapo Juni 2020, vikiwemo vijiji vipya 60 vya Wilaya ya Mkuranga.

Akizungumzia uwajibikaji kwa wafanyakazi wa TANESCO Subira,alisema hasa kada ya maofisa uhusiano na huduma kwa wateja, ijitume, kuhakikisha wanawafuata wateja mahala waliko kwa ajili ya kuwapelekea taarifa mbalimbali pamoja na kupokea kero zao.

Pia aliuelekeza,uongozi wa shirika hilo,kuhakikisha wanafikisha umeme katika mradi wa maji kijiji cha Njopeka,Mkuranga ili kutatua changamoto hiyo kwa manufaa ya wakazi wake.


Subira alieleza,hilo siyo jambo la wizara ya Maji; ni la wizara ya nishati. 
"Nishati tumepewa dhamana ya kuboresha na kuhakikisha huduma nyingine za kijamii zinatolewa katika viwango vyenye ubora,” alisema naibu waziri huyo.

Taarifa ya TANESCO kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani humo inaeleza kuwa, mpaka sasa kazi ya kusambaza umeme imekamilika katika vijiji vyote 15 na kwamba kazi inayoendelea hivi sasa ni kuunganisha wateja.

Vijiji hivyo ni Kinyanya, Jaribu Magharibi, Lumionzi, Mjawa, Ngodai, Mangombela, Bungu A na Bungu B. Vingine ni Motomoto, Tomoni, Kingwila, Mtunda, Kinyamale, Mtawanya kwa Mkengelwa, Bungu Mwongozo na Njopeka.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
Wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...