Muhimbili yawashukuru wachangia damu

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imewaita na kuwashukuru watu waonajitolea kuchangia damu na mazao ya damu mara kwa mara ambayo imekuwa ikitumika kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji.

MNH imewaita wachangia damu na kuwashukuru ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya uchangiaji damu duniani ambayo hufanyika Juni 14, kila mwaka.

Akizungumza leo na wachangia damu kabla ya kuwakabidhi vyeti vya kutambua mchango wao, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa MNH, Dkt. Praxeda Ogweyo amewashukuru kwa kujitolea damu mara kwa mara kila wanapohitajika.

“Mwenyezi Mungu awabariki sana. Pia, tunaomba muwe mabalozi wetu kwa jamii nzima ili nao waige mfano wenu wa kujitolea damu ambayo inatumika kuokoa maisha ya watu wengine. Pia, napenda kuwashukuru wafanyakazi wa kitengo cha damu kwa kutoa huduma bila kuchoka. Bila jitihada zenu, tusingeweza kuwepo hapa siku hii muhimu,” amesema Dkt. Ogweyo.

Dkt. Ogweyo amesema mahitaji ya damu ni makubwa na kwamba uhitaji wa damu MNH ni chupa 100 hadi 120 kwa siku, huku ukusanyaji wa damu kwa siku ukiwa ni chupa 70 hadi 100.

Kutokana na mahatiji makubwa ya damu na mazao ya damu, hospitali imewaomba Watanzania kujenga mazoea ya kuchangia damu na mazao ya damu ili kuboresha benki za damu na mazao ya damu.

“Watanzania wasisubiri kuuguliwa na ndugu ndio waje MNH kuchangia damu na mazao ya damu wanatakiwa kuwa na tabia ya kuchangia damu mara kwa mara ili itumike kuwatibu wagonjwa wakiwamo ndugu wa wagonjwa,” amesema Dkt. Ogweyo wakati akiwashukuru wachangia damu.

Amesema faida ya kuchangia damu mara kwa mara ni mchangiaji kupatiwa damu ambayo itamwezesha kupata damu katika hospitali nchini endapo amepata dharura ya uhutaji pamoja na kujua magrupu ya damu.

Mkurugenzi amesema makundi yenye uhitaji mkubwa wa damu ni wagonjwa wa saratani, watu wanaopata ajali, watoto, kina mama wajawazito na wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Praxeda Ogweyo akimkabidhi Bw. Yusuph Charles cheti cha kutambua uchangiaji wa damu na mazao ya damu mara kwa mara kwa ajili ya kuokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji MNH. Kushoto ni Ofisa Uhusiano wa MNH, Bi. Martha Edward na Mtaalam wa Maabara wa MNH, Bw. John Bigambalaye.
Baadhi ya wachangiaji damu kutoka maeneo mbali mbali jijini Dar es Salaam wakiwa katika tafrija fupi ya kuwashukuru kutokana na mchango wao mkubwa wa kuimarisha benki ya damu na mazao ya damu MNH. 
 Bi. Khalida Ismail mkazi wa Dar es Salaam akikabidhiwa cheti cha kutambua mchango wake katika uchangiaji damu MNH na Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi, Dkt. Ogweyo.
Wachangiaji damu kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja. 
Mkurugenzi wa Huduma Shirikishi wa MNH, Dkt. Ogweyo akiwa katika picha ya pamoja na wachangiaji damu kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...