Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii Nkasi
 MKUU wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda amesema kuwa Wilaya yake imekamilisha ukarabaati wa kituo cha Afya cha Nkomolo na ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari waliofika katika Wilaya ya Nkasi kuripoti habari za miradi ya Maendeleo inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi Rais Dkt.John Pombe Magufuli na kueleza kuwa miradi yote hiyo imejengwa kwa gharama za  sh.Bilioni Mbili.

" Hospitali ya Wilaya inajengwa kwa gharama sh. Bilioni 1.5 na kituo cha Afya Nkomolo kimejengwa kwa gharama ya sh. Milioni 500 ambacho kimekamilika na kitatoa huduma kwa sasa "Amesema Mtanda

Amesema kuwa mara baada ya kukarabati kituo hicho cha Afya wameweza kutoa huduma ya Upasuaji kwa watu sita kwa wakati mmoja jambo ambalo halikuwepo hapo awali.

"Kwa sasa tuna chumba cha kuhifadhia maiti na majokofu sita ambayo awali hayakuwepo na wakazi wa hapa walikuwa wanalazimika kutembea hadi Sumbawanga kwa ajili ya kuhifadhi maiti" ameeleza.

Aidha amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 1979 haikuwahi kuwa na chumba cha kuhifadhia maiti, lakini kutokana na jitihada za serikali ya awamu ya tano,Nkasi imeorodheshwa kati ya wilaya ambazo zimefaulu kwa kupiga hatua kimaendeleo ikiwemo sekta ya elimu na afya.

Amesema kuwa kuwa kwa kipindi chote hicho Wilaya hiyo ilikuwa haina Hospitali ya Wilaya lakini katika awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli, Nkasi imepata Hospitali mpya.

Mtanda amesema licha ya mafanikio hayo, Mganga Mkuu wa kituo cha afya Nkomolo Everada Sanane amesema bado kuna uhitaji wa watumishi kutokana na idadi ya wagonjwa inavyoongezeka na ameishukuru serikali kwa hatua ilizozipiga katika kuboresha sekta mbalimbali Wilayani humo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda akizungumza na Waandishi wa Habari wakati kuhusiana  na   Miradi ya Maendeleo katika Wilaya hiyo  iliyofanywa katika Serikali ya awamu ya tano.
 Kituo cha Kituo cha afya kilichojengwa katika serikali ya awamu ya Tano na kutatua changamoto ya huduma za afya
 Mganga Mkuu wa Kituo Cha Afya Nkomolo,Everanda Sanane akieleza changamoto zinazopatikana katika kituo hicho wakati waandishi wa habari walipofika kituoni hapo.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda akionyesha majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Nkasi inayojengwa kwa gharama za Bilioni 1.5.
 Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda akizungumza na Mmoja wa Wagonjwa waliofanikiwa kupata matibabu katika kituo cha afya Nkomolo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...