Ofisi ya Makamu wa Rais imeshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza Juni 16 hadi Juni 23 mwaka huu kwa kutoa elimu kwa wananchi na kushiriki shughuli za kijamii. 

Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashambwa amesema shughuli mbalimbali za kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano na Mazingira zimeanza kufanyika kupitia vyombo vya habari. 

Mwashambwa alisema tathmini ya kampeni ya marufuku ya mifuko ya plastiki na masuala yanayotakiwa kufanyika baada ya hatua hiyo pamoja na kuendeleza kampeni ya matumizi ya mifuko mbadala imeanza kufanyika. 

Aliongeza kuwa wananchi wataelimishwa kuhusu aina za mifuko mbadala yenye ubora unaotakiwa kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa miongozo. 

"Katika kwenda sambamba na sera ya viwanda wananchi watapata wasaa wa kufahamu tathmini ya athari kwa mazingira ili kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafanikiwa na pia wataelimishwa kuhusu wajibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais katika matumizi salama ya bioteknolojia ya kisasa pamoja na bidhaa au viumbe watokanao na teknolojia hii," alisema. 

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi huyo, Wiki ya Utumishi wa Umma itatumika katika kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Muungano kwa ujumla ikiwemo mafanikio katika kuondoa changamoto zake. 

Maadhimisho haya ni kwa mujibu wa kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kushiriki shughuli mbalimbali zinazohusu Utumishi wa Umma hivyo aliwataka wananchi waendelee kufuatilia vyombo mbalimbali vya habai kupata elimu. 

Kwa mwaka huu kauli mbiu ni Uhusiano kati ya Uwezeshaji wa Vijana na Usimamizi wa Masuala ya Uhamiaji; Kujemga Utamadni wa Utawala Bora, Matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utaoaji Huudma Jumuishi.
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Ofisi ya Makamu wa Rais, Samuel Mwashambwa 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...