Na Emanuel Madafa, Mbeya .
Dhamira ya Rais Dk. John Magufuli ya kuwapatia wananchi huduma nzuri, itafanikiwa endapo viongozi wenye dhamana ya kuisimamia Serikali hawatakuwa wasanii wa kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa Inyala kwa gharama ya Sh1.5 bilioni na kuonekana kuridhishwa na kasi ya ujenzi wake.

Chalamila amesema Rais Magufuli ana nia njema kwa Watanzania lakini baadhi ya wasaidizi wake ndio wanaomuangusha na ndio sababu inayomfanya kupangua pangua safu ya uongozi wake.

Amesema endapo viongozi walioaminiwa wakiwa ni wasanii katika kusimamia na kutekeleza maazimio ya Rais Magufuli hawatakuwa wamembeba wala kumuwakilisha vyema.

“Tukiacha usanii na kuweka kando rushwa na ufisadi…tutakuwa tumembeba vizuri Rais katika kuwatumia Watanzania.  Kwa hiyo hospitali hizi zote za mkoa wetu wa Mbeya zinaenda vizuri sana na hii inadhihirisha sisi viongozi wake ni wasafi na tunasimamia vyema fedha na hatujawa wasanii  na ndio maana majengo yanaonekana lakini kama tungekuwa wasanii nina amini  tungekuwa tumefukuzwa kabisa”.

Amesema Serikali imetoa zaidi ya Shilingi 6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za wilaya tatu ambazo ni Mbarali, Busokelo na Mbeya na vituo vya afya 14 kwa mkoa mzima wa Mbeya 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Steven Katemba amesema fedha hizo Sh1.5 bilioni zimewezesha kujenga majengo saba  ya kutolea huduma  zote muhimu katika hospitali hiyo.

Amesema pia halmashauri yake  imetoa Sh60 milioni ambazo zitasaidia kujenga nyumba mbili za watumishi lakini wananchi wametoa ushirikiano mzuri kwenye ujenzi huo ikiwamo kutoa eneo la ardhi ili ijengwe hospitali hiyo.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila leo wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa eneo la Inyala ,kwa gharama shilingi Bilioni 1.5
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (mwenye kofia), Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika,Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba(Katikati) na Mganga Mkuu Wilaya ya Mbeya Dkt  Yahaya Msuya ,wakikagua Maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya ambayo inajengwa eneo la Inyala kwa gharama ya shilingi Bil 1.5
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila (katikati) ,Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (Kushoto) na Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbeya Stephan Katemba wakiwa katika eneo la ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Mbeya ambayo inajengwa kwa shilingi Bilioni 1.5.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...