*Ni yale aliyoyatoa wakati wa kikao cha wafanyabiashara 
*Yatangaza kuwafikisha Mahakamani watumishi wa TRA, Polisi 
*Yapeleka timu kuwachunguza askari walionyanyasa wafanyakazi Moro


Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa(TAKUKURU)imesema tayari imeanza utekelezaji wa maagizo ya Rais Dk.John Magufuli ambayo ameyatoa Juni 7,2019 wakati wa kikao kazi kati yake na wafanyabishara nchini .

Kwa mujibu wa TAKUKURU imesema imeanza kufanyia kazi na kuchukua hatua mbalimbali za uchunguzi kuhusu tuhuma za mfanyabishara aliyeuzuliwa mzigo wake tangu mwaka 2016.

Katika kutekeleza maagizo hayo TAKUKURU leo Juni 10,2019 imesema itawafikisha mahakamani watumishi watatu waliohsika na ukamataji na uzuiaji wa mzigo wa mfanyabiashara Ramadhan Hamisi Ntunzwe kwa makosa ya rushwa.

Taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Diwani Athumani kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Juni 10 , 2019 amewataja watumishi hao ni Charity Ngalawa muajiriwa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Askari Polisi H 4086 PC Simon Sungu pamoja na askari polisi H4810 PC Ramadhan Uweza ambao wote wanatoka Kituo cha Polisi Oyestarbey Mkoa wa kinondoni jijini Dar es Salaam.

"Watuhumiwa hao kwa pamoja watafafikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam ili kujibu shitaka la kuomba rushwa ya sh.milioni 20 kutoka kwa mfanyabiashara wa Kariakoo Ramadhan Ntuzwe kinyume na kifungu 15(1)(a)cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

"Katika uchunguzi huo TAKUKURU imebaini watuhumiwa hao waliomba kiasi hicho cha fedha kama kishawishi ili waweze kuachia mzigo wa mfanyabishara huyo ambao waliukamata kwa madai ya kufanya udanganyifu wa kiwango cha biadhaa alizonazo.

"Hivyo kuathiri ukadiriaji wa kodi.Pia watuhumiwa wengine waliohusika kwa namna moja au nyingie katika suala hili wanaendelea kuchunguzwa,"amesema Mkurugenzi huyo wa TAKUKURU.

Kuhusu ukadiriaji wa kodi kwa bidhaa za mmiliki wa kampuni Steps Entertaiment ni kwamba watumishi wa nne wa TRA Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam wanaohusika na ukaguzi na ukadiriaji wa kodi wanashikiliwa na TAKUKURU kwa auchunguzi dhidi ya ukaguzi na ukadiariaji wa kodi walioufanya kwa bidhaa za mfanyabiashara Dilesh Solanki ambaye ni mmiliki wa kampuni hiyo iliyoko jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Athumani amesema watuhumiwa hao wa TRA wanachunguzwa kwa kosa la kutumia madaraka yao kinyume na kifungu cha 31 cha sheria ya kuzuia na kupamba na rushwa namba 11, 2017.

"Wanadaiwa kutoa makadirio ya juu ya kiasi cha Sh.bilioni 3 na milioni 100 kama kodi za bidhaa mbalimbali za mfanyabiashara huyo jambo ambalo linaashiria ushawishi wa rushwa.Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii bado unaendelea na taarifa kamili itatolewa uchunguzi huu utakapokamilika,"amesema.

Wakati huo huo amesema TAKUKURU Makao makuu imeongeza nguvu kuchunguza tuhuma za unyanyasaji na madai ya hongo kwa wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu Athumani amefafanua tuhuma hizo zinadaiwa kufanywa na askari Polisi dhidi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Leaf Tobacco Company na kwamba timu ya uchunguzi tayari TAKUKURU makao makuu imeongeza nguvu timu ya uchunguzi na kisha taarifa itatolewa.

Wakati wakiendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma hizo, TAKUKUKURU kupitia Mkurugenzi Mkuu wake imetoa rai kwa wananchi kuendelea kumuunga mkono Rais Dk.John Magufuli ambaye siku zote amekuwa mstari wa mbele katika kuongoza mapambano dhidi ya rushwa.

"Pia tunawasihi wananchi kuwa tayari kutoa ushahidi katika kesi mbalimbali zinazochunguzwa na TAKUKURU ili kuunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya rushwa nchini,"amesema Athumani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...