Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe. George Mkuchika (Mb), akizungumza na
vyombo vya habari jijini Dododma kuhusu Maadhimisho ya Wiki ya
Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst)
Mhe. George Mkuchika (Mb), alipokuwa akizungumza nao kuhusu
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2019.


Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Ummana Utawala Bora, inaratibu maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma

Barani Afrika kwa mwaka 2019 ambayo hufanyika mara moja kila baada ya
miaka miwili katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, Waziri wa Nchi, Ofisi yaRais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt (Mst) Mhe.

George Mkuchika amesema maadhimisho hayo kwa mwaka huu,yanatarajiwa kufanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 21 hadi 23 Juni, 2019.Mhe. Mkuchika amefafanua kuwa, malengo ya kuadhimisha siku hii kilabaada ya miaka miwili, ni kuziwezesha nchi wanachama wa Umoja wa Afrikakubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Usimamizi wa Utumishina Utawala hususan mafanikio na changamoto ili kuzitumia kama chachu yakuboresha utoaji huduma kwa umma.

Mhe Mkuchika amesema, taasisi zitakazoshiriki katika maadhimisho hayo, nizile ambazo huduma zake zinalenga moja kwa moja kaulimbiu ya mwaka huuinayosema “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa
masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya
TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi,” hivyo kuzitaka
taasisi hizo kuwa mabalozi wazuri katika kuiwakilisha nchi yetu.

Mhe. Mkuchika amezitaja shughuli zitakazofanyika kuwa ni pamoja na
maonyesho ya kazi za ubunifu zilizofanywa na Taasisi kulingana na Kauli
Mbiu, mdahalo kuhusu masuala ya Uwezeshaji wa Vijana, Utawala Bora,
matumizi bora ya TEHAMA, Ubunifu katika utoaji Huduma Jumuishi na namnabora ya kujenga maadili katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Mkuchika amesema, katika maadhimisho ya kitaifa, ofisi yake
imewaelekeza Watendaji wa Taasisi za Umma, kukutana na watumishi katikamaeneo yao ya kazi ili kusikiliza maoni na changamoto wanazokutana nazokatika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kukutana na wadauwa nje kwa lengo la kupata mrejesho wa huduma wanazozitoa.
Mhe. Mkuchika ameongeza kuwa, ili kujenga mahusiano mazuri na jamii,
Taasisi za Umma zinaweza kuadhimisha wiki hiyo kwa kufanya shughuli za
kijamii kama vile za usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali hususan
hospitali, sokoni na katika fukwe za mito na bahari zilizo jirani na maeneo yaoya kazi.

Sanjari na hayo, Mhe. Mkuchika ameziagiza Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka
za Serikali za Mitaa na Taasisi zote za Umma kuwasilisha taarifa ya namna
walivyoshiriki maadhimisho hayo kwa Makatibu Wakuu wa Wizara ambao
wataunganisha taarifa hizo na kuziwasilisha kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma ili Serikali iweze kutumia taarifa hizokuboresha utendaji kazi.

Aidha, Mhe. Mkuchika amewapongeza watumishi wote wa umma nchini kwa
kutekeleza wajibu wao ipasavyo na kuwahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa
manufaa na maendeleo ya Taifa letu.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma husherehekewa na Nchi
Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 Juni
kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo
ya Nchi zao na Bara la Afrika kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...