Upanuzi wa New Bagamoyo road awamu ya pili unaendelea,Upanuzi wa barabara hiyo ukikamilika utapunguza adha kubwa ya msongamano wa magari wakati wa kuingia na kutoka katikati ya jiji.

Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Maendeleo (JICA), iliipatia Tanzania ruzuku ya Yen bilioni 3.78 sawa na Shilingi bilioni 77.3 kwa ajili ya upanuzi wa barabara ya New Bagamoyo, kuanzia Morocco hadi Mwenge, Jijini Dar es Salaam.

Makubaliano ya msaada huo yalitiwa saini Februari 28, 2018, Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, kwa niaba ya Serikali, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida na kushuhudiwa na Mwakilishi Mkazi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Japani (JICA), Toshio Nagase na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini-Tanroads, Mhandisi Patrick Mfugale.

Mradi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 4.3 utahusisha barabara yenye njia nne pamoja na kuanza kwa awamu ya nne ya ujenzi wa barabara itakayotumiwa na mabasi ya mwendo wa haraka (BRT phase IV).

Akizungumza baada ya kutiwa saini wa makubaliano hayo, Bw. Doto James alisema kuwa barabara hiyo ikikamilika itasaidia kutatua changamoto ya msongamano wa magari yanayotoka na kuingia katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

“Upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo si tu kwamba utaondoa msongamano wa magari, bali pia ni kiungo muhimu cha Bandari ya Bagamoyo ambayo itarahisisha usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma kutoka Jiji la Dar es Salaam, mkoa wa Pwani na mikoa mingine nchini” Alisema Bw. Doto James.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...