Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Katika kuadhimisha wiki ya Utumishi kwa Umma Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Kanda ya Mashariki kwa kushirikiana na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa  NIDA pamoja na kitengo cha polisi makosa ya mtandaoni wamefungua kituo cha pamoja kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usajili laini  za simu kwa kutumia alama za vidole.

Maadhimisho hayo ni muhumu kupata huduma za mawasiliano katika mwamvuli mmoja pamoja na kupunguza gharama za usafiri.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho hayo  Kaimu Mkuu wa TCRA Kanda ya Mashariki  Mhandisi Jumanne Ikuja amesema kuwa usajii huu utasaidia  kukomesha wizi wa mtandaoni kwani kila mwananchi atatakiwa kumiliki laini moja kwa kila Mtandao wa kampuni ya simu.

Aidha amewata wananchi wanaopoteza vitambulisho vyao kuhakikisha kuwa wanaripoti polisi ili kuweza kurudishiwa vitambulisho vingine katika kuepuka  kutumiwa kwenye matukio ya kihalifu.

Mhandisi Ikuja  amewasisitiza wananchi kufika katika viwanja vya mnazi ili kupatiwa huduma mbalimbali zinazohusiana na Mawasiliano kwani zoezi hilo ni la wiki moja kuanzia Juni 17- 21 mwaka huu.

Kwa upande wake  Mkaguzi Msaidizi wa polisi Kitengo Cha makosa ya mtandaoni Inspekta Edga Masawe amewatahadharisha wa anchi kuacha kutumia simu ambazo wamezinunua kiholela haswa kutoka kwa watu pamoja na zile wanazoziokota ikiripotiwa ni unachukuliwa kama mhalifu.

Hata hivyo amesema kuwa kupitia maadhimisho ya wiki ya utumishi watatoa elimu kwa wananchi kuhusu sheria za mtandaoni pamoja na  madhara ya matumizi mabaya ya mtandao ikiwemo matumizi ya lugha isiyokuwa na staha na picha zisiokuwa na maadili na maneno ya uchochezi.
 Kaimu Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Jumanne Ikuja akizungumza na waandishi habari kuhusiana na TCRA na wadau wengine kuungana katika kutoka huduma za usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Makosa Mtandaoni Edga Massawe akizungumza kuhusiana na Makosa Mtandaoni kwa waandishi habari na kutaka wananchi waende kupata maelezo  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Wananchi wakipata huduma katika kampuni za simu.
 Wananchi wakipata huduma katika kampuni ya simu ya TTCL katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 Afisa wa TCRA Kanda ya Mashariki Annastella Mchomvu akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda TCRA katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.Picha mbalimbali za matukio katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...