Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) wamekabidhi rasmi majengo ya Shule ya Sekondari ya Wasiichana Kondoa kwa uongozi wa Halmashauri ya Mji Kondoa baada ya kukamilisha ukarabati mkubwa.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Shule hiyo na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji, Mamlaka ya Elimu Tanzania, Bodi ya Shule na uongozi wa shule.

Akikabidhi mradi huo Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Tija Ukondwa alisema kuwa mradi huo umefanikiwa kwa viwango vya hali ya juu kwasababu wasimamizi wa mradi waliweka tamaa nyuma na kutanguliza uzalendo hadi wanakabidhi majengo hayo.

“Fedha hizi zimetolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania lakini ni kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kuwa shule kongwe zinafanyiwa ukarabati hivyo ni jukumu lenu kuitunza shule hii ili itumike kwa kipindi kirefu.”Alisema Tija

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kaunga Amani aliwashukuru TEA kwa kuichagua shule ya Wasichana Kondoa kwa kuwa shule zipo nyingi nchini ila wakaona shule hiyo inafaa katika awamu hii.

“Nichukue fursa hii kuwashukuru pia bodi ya shule kwa usimamizi mzuri maeneo mengine wengi wanaishia kuvunja bodi sababu ya maslahi ila hapa hatukuliona hilo, pia washauri wa mradi huo Chuo Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya walifanya kazi nzuri ya usimamizi kazi ambayo tunafanya nao kwa kipindi cha pili sasa.”Alisema Kaunga

Naye Mwenyekiti wa bodi ya Shule Emanuel Mkubwa alisema ukarabati huo ulikuwa mgumu ila usimamizi ulikuwa mkali kuhakikisha malengo yanatimia na yametimia kutokana na ushirikiano uliokuwepo kati ya uongozi wa shule na Halmashauri.

“Pongezi nyingi ziende kwa Mhe.Rais Dkt. John Magufuli kwa kutuwezesha shule yetu kukarabatiwa na leo lengo lake limetimia na katika kipindi chote hicho cha mradi ajira zilipatikana na mzunguko wa fedha uliongezeka tunashukuru sana ila tunaomba pia mtusaidie kisima cha maji na ukarabati wa nyumba za walimu ili kuzidi kuongeza hali ya ufaulu shuleni hapa.” Alisema Emanuel

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...