Na Grace Semfuko,MAELEZO

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema inayo maabara ya kisasa ya upimaji wa usalama wa mazao ya Chakula ili kuondokana madhara yatokanayo na ulaji wa vyakula vizivyopimwa yakiwepo magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula vyenye Sumu kuvu.

Aidha Mamlaka hiyo imejipanga kupambana na magonjwa yanayosababishwa na ulaji wa vyakula hivyo ambayo yana athari kubwa kwa afya za binaadamu ikiwepo udumavu na vifo.

 Hayo yalibainishwa na Mkaguzi wa chakula Mwandamizi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania TFDA Dkt Analice Kamala wakati akiwasilisha mada juu ya uchafuzi wa Sumukuvu madhara yake kwa afya na jinsi ya kudhibiti katika Semina ya kuwajengea uwezo Waandishi na Wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Dkt Kamala alisema alisema maabara za kisasa za upimaji wa vyakula zilizopo kwenye Mamlaka hiyo zina uwezo wa kisasa wa kubaini magonjwa au vimelea vya fangas ambavyo huathiri vyakula hususa vilivyohifadhiwa kwenye maeneo yasiyo salama ikiwepo sehemu ya  unyevu unyevu,joto na wadudu wa nafaka.

“ Niwahakikishie tu watanzania wenzangu kuwa vyakula vinavyopimwa kwenye maabara hii ni salama, hakuna kinachopita hapa kikiwa na madhara, kitatupwa tu, tuzingatie usalama wa vyakula na tutumie vyakula vilivyopimwa alisema Dkt Kamala.

Aidha katika hatua nyingine Dkt Kamala aliwataka Wanawake wanaonyoshesha nchini kuwa waangalifu katika uandaaji na matumizi ya vyakula wanavyotumia ili kuepukana na madhara ya Sumukuvu iliyopo kwenye baadhi ya vyakula vya nafaka ambayo inadaiwa kuwa na madhara kwa binaadamu na wakati mwingine husababisha vifo.

Dkt Kamala alisema iwapo Mama anayenyonyesha atatumia vyakula vyenye sumukuvu anasababisha madhara makubwa kwa Mtoto ikiwepo Udumavu, Vifo na Magonjwa ambayo yanaathiri ukuaji wa mtoto.

“Wanawake wanaonyonyesha ni muhimu kuzingatia uandaaji wa vyakula kwani watoto hula vyakula hivyo kupitia kwenye Maziwa ya Mama na hivyo kuathiri mfumo mzima wa ukuajiƤlisema Dkt Kamala.

Aidha pia Dkt Kamala alisema ulaji wa mazao ya mifugo iliyotumia vyakula vilivyoathiriwa na sumu kuvu pia inaweza kuathiri afya za binaadamu.

Alisema Sumu kuvu inaathiri ini na Figo na kusababisha ugonjwa wa manjano na wakati mwingine kuvuja damu kwenye maeneo ya wazi,kuharisha na kuhisi kichefuchefu na dalili zake huanza kuonekana baada ya wiki mbili.

Ugonjwa huo kwa Nchini Tanzania ulilipotiwa na Wizara ya Afya Juni 13 mwaka 2016 Mkoani Dodoma ambapo ilibainika kuwepo kwa watu 68 kwenye familia 42 kuugua magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye sumu kuvu na kati yao watu 20 sawa na asilimia 30 walipoteza maisha.
Ofisa Mwandamizi wa Uchanganuzi wa Hatari zitokanazo na Chakula kutoka (TFDA) Dkt. Analice Kamara akifafanua moja ya Mada kuhusu Madhara ya Sumu kuvu mbele ya Waandishi wa Habari katika kikao kazi  cha  kuwajengea uwezo waandishi na wahariri wa Habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula ,iliyofanyika  leo katika ukumbi wa  Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv) 

Meneja Mawasiliano na  Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) , Bi. Gaudensia  Simwanza akifafanua jambo katika kikao kazi cha kuwajengea uwezo waandishi  wa habari katika kuelimisha jamii kuhusu usalama wa chakula iliyofanyika katika ukumbi wa   Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kikao kazi hicho kilichofanyika katika ukumbi wa  Chuo cha Uvuvi Mbegani wilaya ya Bagamoyo mko wa Pwani.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...