Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) inafanya maonesho ya Utumishi wa Umma-siku saba mfululizo ambayo yatafanyika ndani ya makao makuu ya wakala huo kuanzia Juni 17 hadi 23,mwaka huu wa  2019. 

Maonesho hayo ambayo yatazinduliwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  Profesa Dos Santos Silayo yamebeba kaulimbiu inayosema “Uhusiano kati ya uwezeshaji wa vijana na usimamizi wa masuala ya uhamiaji: Kujenga utamaduni wa Utawala Bora, matumizi ya TEHAMA na ubunifu katika utoaji wa Huduma Jumuishi,”.

Akizungumza  leo  jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma Saidizi TFS,  Emanuel Wilfred amesema TFS itafanya maonesho hayo kwa kipindi cha siku saba kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa 12 jioni ili wananchi waone shughuli zinazofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. 

“Wananchi watajionea na kuelimika na mambo mbalimbali yanahohusu uhifadhi wa misitu,ufugaji nyuki, na biashara ya mazao ya misitu na utalii na pia kuwapa fursa wananchi kutoa maoni na malalamiko juu ya huduma tunazotoa,’’amesema Emanuel. 

Kupitia kauli mbiu hiyo amesema TFS itaeleza ni namna gani wanapambana na vitendo vya uharibifu wa misitu na udhibiti wa ukusanyaji mapato katika utoaji wa huduma kwa wananchi na pia kuwaeleza wananchi mipango iliyopo katika kuhakikisha kunakuwa na matumizi endelevu ya mazao ya misitu na nyuki. 

Katika maonesho hayo watalaam waliobobea kutoka maeneo mbalimbali ya Wakala watakuwepo ambao ni maafisa misitu, maafisa nyuki, maofisa masoko, watoa leseni, na wataalamu wa Tehama ili kukutana na wananchi watakaojitokeza. 

Maadhimisho hayo ni moja ya matukio katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU) ambapo nchi wanachama huadhimisha kwa kufanya maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi zake na pia kongamano kuhusu masuala ya Utumishi wa Umma. 

Pi maonesho hayo huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejiment ya Umma na Utwala Bora ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia 16 hadi 23 Juni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...