Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
ALIYEKUWA  Rais wa shirikisho la mpira barani Ulaya (UEFA) kwa mwaka 2007-2015, mchezaji wa zamani wa Ufaransa na mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon I'or Michel Platini anahojiwa na mamlaka za uchunguzi wa masuala ya ufisadi na rushwa kwa kile kilichoelezwa ni kuipa nafasi Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la duniani mwaka 2022 vyombo vya habari nchini Ufaransa vimeripoti.

Michel (63) ambaye aliwahi kuwa Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya na baadaye kufungiwa kujihusisha na soka mwaka 2015 kwa kile kilichoelezwa ni ukiukwaji wa kanuni maadili.

Wakati wa kutafuta mwenyeji wa mashindano hayo ya kidunia mwaka 2010 Qatar iliibwaga Marekani, Australia, Japan na Korea Kusini. Michel amekana mashtaka hayo aliyohojiwa huko Nanterre magharibi wa mji mkuu wa nchi hiyo Paris.

Imeelezwa kuwa shutuma dhidi yake zilianza kuchunguzwa miaka miwili iliyopita na katika sakata hilo Sepp Blatter aliyewahi kuwa Rais wa shirikisho la mpira duniani (FIFA) ambaye pia alipigwa marufuku kujihusisha na soka alihojiwa mwaka 2017.

Aidha FIFA imetakiwa kuifanyia uchunguzi wa kina Qatar kuhusiana na sakata hilo.

Michel Platin alikata rufaa mara baada ya kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka  ambapo alipunguziwa adhabu hadi kufikia miaka minne ambayo anaimaliza Oktoba mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...