Afisa Madini mkazi mkoa wa Njombe na Iringa Wilfred Machumu
katikati akiambatana na Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris
Kikula wa kwanza kulia wakiingia kukagua soko la madini ya
Dhahabu na Vito mkoa wa Iringa. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula wa kwanza kushoto,
Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma wa nne kulia
wakiwa kwenye kikao na mwenyeji wao mkuu wa mkoa Ruvuma
Christina Mndeme kuhusu ukusanyaji wa maduhuli ya serikali kupitia
sekta ya madini. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula mwenye kofia akiwa
kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wa kampuni ya Thomas G.
Masuka & Partners kwenye mgodi wa Nyakavangala Isimani mkoani
Iringa. 
Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula na Kamishna wa
Tume hiyo Prof. Abdulkarim Mruma wakiwa chini kwenye mgodi wa
kampuni ya TANCOAL inayo zalisha makaa ya mawe
walipotembelea eneo la uzalishaji mgodini hapo. 




Na Issa Mtuwa “WM” Iringa

Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amekemea na kutoa onyo
kwa Wachimbaji na wanunuzi wa madini nchini kuacha tabia ya kufanya
biashara ya madini nje ya masoko yaliyoteyari na yanayoendelea
kuanzishwa mikoa yote hapa nchini. 

Prof. Kikula amesema hayo Juni 15, 2019 muda mfupi mara baada ya
kukagua soko la madini mkoani Iringa ambako hakuridhishwa na takwimu
za uuzaji wa madini ya dhahabu katika soko hilo kuwa spidi ni ndogo
akitolea mfano wa takwimu zilizotolewa na Mkaguzi wa Madini kituo cha
Iringa Severine Haule kuanzia tarehe 30 Mei, 2019 hadi tarehe 14 Juni,
2019 ni gram 92 tuu za dhahabu zimezalishwa na kupita sokoni hapo. 

Amesema serikali haina mzaha kuhusu suala hilo na yeyote atakae kutwa
anafanya biashara ya madini nje ya masoko rasmi atakumbana na mkono
wa sheria ikiwemo kutaifishwa madini na kila aina ya raslimali iliyotumika
kuwezesha ufanyikaji wa biashara hiyo, hivyo ametoa wito kwa wadau
wote kujiepusha na utoroshaji wa madini sambamba na kufanya biashara
nje ya Masoko. 

Ameongeza kuwa, jicho la serikali linaona mbali hivyo asijidanganye mtu.
Amesema kuwa ziko taarifa za ujanja ujanja kufanya biashara ya kuuziana
madini usiku wilayani Tunduru, wengine kutorosha madini kuelekea Malawi
kwa wilaya ya Songea na Mbinga, na Iringa wachimbaji wadogo, wanunuzi
wa kati (Brokers) na wanunuzi wakubwa (Dealers) kuuziana madini kwa siri
kutofikisha madini kwenye soko. Amesema taarifa zote hizo serikali inazo
hivyo amewaomba wadau wote wanaohusika na michezo hiyo waache
mara moja na kama wataendelea wajue siku zao si nyingi hivyo
wasijitafutie matatizo wakaacha familia zao bila sababu. 

Wakati huo huo Mwenyekiti ameendelea kuwasisitiza watumishi wa Tume
hiyo mikoa yote nchini kuzingatia uadilifu na kwamba kamwe wasikubali
kushawishika kwa rushwa. 

Amesema laiti kama yeye angekuwa mwepesi wa kupokea rushwa pengine
asingekuwa anaendelea kumsaidia Rais Magufuli kuwatumikia Wananchi
kwani yapo majaribu mengi na majaribio ya watu kumpelekea vifurushi na
mabegi ya fedha lakini hajawahi kuingia katika mitego hiyo na hajawahi pokea rushwa hata siku moja katika miaka 46 ya maisha yake yote ya
utumishi wa umma. 

Amewambia watumishi hao kuwa wakae wakijua wale watakao waletea
fedha hiyo siri haitabaki kwa mtu mmoja lazima itavuja na huo ndio
mwanzo wa kuharibu jina lake hivyo wasikubali rusha ni hatari. 

Mwenyekiti Prof. Idris Kikula na Kamishna wa Tume ya Madini Prof.
Abdulkarim Mruma wamehitimisha ziara yao katika mikoa ya Lindi, Mtwara,Ruvuma, Njombe na Iringa ambako walikuwa wanakagua shuguli zamadini, kuhimiza ulipaji wa maduhuli ya serikali, utatuzi wa migogoro,
kusikiliza kero na kutatua, kuongea na wafanyakazi wa tume ya madini,
wachimbaji, wafanyabiashara wa madini na kuognea na viongozi wa
serikali ngazi ya mikoa na wilaya. 

Yaliyojiri kwa ujumla katika ziara hiyo ni pamoja na; kilio cha wachimbaji
wadogo katika mikoa mbalimbali kutozwa kodi zaidi na Halmashauri za
wilaya na vijiji kinyume cha sheria ya madini, ufinyu wa bajeti, uhaba wa
watumishi na vitendea kazi kwa ofisi za tume ya madini mikoani,
ucheleweshaji wa utolewaji wa leseni za uchimbaji kwa wachimbaji
wadogo, ulipaji wa maduhuli ya serikali, uuzaji wa madini kwenye masoko
rasmi, uadilifu na kuepuka rushwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...