Umoja wa makanisa ya Kipentecoste Mkoani Shinyanga wamefanya mazoezi na kuchangia damu salama, ili kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya tano kwa kuimarisha afya za wananchi, pamoja na kuokoa vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi kwa sababu ya kumwaga damu nyingi.

Mazoezi hayo yamefanyika leo Juni 15, 2019 kwenye uwanja wa wamichezo wa Sabasaba, na kuongozwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga, mhe. Jasinta Mboneko, ambayo yalianza kwa matembezi na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga na kuhitimishwa kwa kuchangia damu salama. Akizungumza kwenye mazoezi hayo, mwenyekiti wa umoja wa makanisa hayo ya Kipentecoste mkoa wa Shinyanga,Askofu Elias Madoshi, amesema wao kama viongozi wa kidini wameona ni vyema kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi pamoja na kuchangia damu salama. 

Amesema juhudi za serikali ya awamu ya tano zinapaswa kuungwa mkono, ambapo wananchi wakiwa na afya mgogoro kamwe hawataweza kufaya shughuli za uzalishaji mali, na hatimaye nchi kushindwa kukua kimaendeleo na kufikia kwenye uchumi wa kati. “Sisi kama Umoja wa makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga CPCT kwa kushirikiana na umoja wa makanisa ya Kiinjili CCT, Tumeamua kuungana na Serikali kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi ili wawe na afya imara, pamoja na kuchagia damu salama ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vikonavyo na uzazi kwa kumwaga damu nyingi wakati wa kujifungua”amesema Madoshi. 

“Hivyo tunatoa wito kwa wananchi mkoani Shinyanga wajikite kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao pamoja na kujitoa kuchangia damu salama, ambayo itaokoa maisha ya wagonjwa wenye uhitaji wa damu ikiwamo na kumaliza vifo vya uzazi vitokanavyo na umwagaji damu nyingi,”ameongeza. Naye mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, amepongeza Umoja huo wa makanisa ya Kipentecoste kwa kutoa hamasa ya wananchi kushiriki kufanya mazoezi pamoja na uchagiaji wa damu salama. 

Amesema mazoezi hayo yalizinduliwa na makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambayo yatafanyika kila Jumamosi ya pili ya mwisho wa mwezi, na kuwasihi watumishi wa serikali kuwa mfano wa kuigwa kushiriki kwenye mazoezi hayo na siyo kuwa wategeaji, ambapo ataanza kuwa anapitisha daftari la ukaguzi wa majina ya watumishi. 

Kwa upande wake mratibu wa Damu salama mkoani Shinyanga,Dkt. Joel Mdale, ametoa shukrani kwa umoja huo wa makanisa ya kipentecoste kwa hamasa hiyo ya uchangiaji wa damu salama, jambo ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa damu kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa, na hatimaye kuokoa vifo vya wagonjwa wenye uhitaji wa damu wakiwamo wajawazito. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akiwataka wananchi kuendelea kufanya mazoezi ambayo yatawasidia kuimarisha afya zao. Picha na Marco Maduhu - Malunde1 blog. Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentecoste mkoani Shinyanga Askofu, Elias Madoshi, akielezea namna walivyohamasika kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya Tano, kwa kufanya mazoezi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchagia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko katikati mwenye kofia akiongoza mazoezi kwa kutembea kwa miguu pamoja na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga. Mazoezi yakiendelea kwenye uwanja wa Sabasaba mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kutembea na kukimbia kwa kuzunguka mji wa Shinyanga. Viongozi wa dini kutoka makanisa ya kipentecoste mkoani Shinyanga wakiwa na wananchi pamoja na watumishi wa Serikali kwenye mstari kwa ajili ya kuchangia damu salama kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Mratibu wa damu salama mkoani Shinyanga Joeli Mdale akimtoa damu Askofu Josephat Msila kutoka kanisa la Kipentecoste (TMRC) Ndembezi mjini Shinyanga. Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea. Askofu Josephat Masaga kutoka kanisa la (TAG) Shinyanga, akiombea amani mkoani Shinyanga katika kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...