Na Editha Karlo wa blog ya jamii.Kigoma

MRATIBU Mkazi umoja wa mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez amesema umoja wa mataifa uko tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto ambavyo hushusha utu wao.

Alvaro ameeleza vitendo vya ukatili si swala la Tanzania pekee ni swala la kiulimwengu hivyo mashirika mbalimbali yanapaswa kushirikiana kukomesha vitendo hivyo na kuwa wako tayari kuendelea kushirikia na serikali katika hilo.

Hayo ameyasema leo akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na mradi wa Kigoma Joints Program(KPJ) baada ya kukagua ofisi ya dawati la jinsia la polisi Mkoani Kigoma lililojengwa kwa ufadhili wa kupitia mradi wa Kigoma pamoja(KJP).

Pia ameushukuru uongozi wa Mkoa wa Kigoma kwa ushirikiano wanaoutoa kwenye programu ya Kigoma pamoja na kusema wataendelea kuwa marafiki wa serikali ya Tanzania hususani Mkoa wa Kigoma.

Mwakilishi wa jeshi la polisi kutoka dawati la jinsia WP Anastazia Daud amesema kwasasa jamii imeendelea kuwa na mwamko wa kutoa taarifa matukio yanayohusiana na ukatili ambapo kwa wilaya ya Kigoma bado kumekuwa na matukio ya ukatili na mashambulio ya aibu.

"Kupitia elimu mbalimbali zinazoendelea kutolewa ssa hivi jamii imekuwa na mwitikio mkubwa wa kutoa taarifa ya matukio ya ukatili kwa wanawake na watoto"alisema.Mkuu wa mkoa wa Kigoma mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga akahimiza jamii kuacha kuona aibu kutoa taarifa pindi zinapokumbana na unyanyasaji wa kijinsia.

"Wapo akina baba wanapigwa huko na kunyanyaswa na wake zao mje mtoe taarifa hapa malalamiko yenu yatafanyiwa kazi"alisema.

Maganga aliushukuru umoja mataifa(UN)kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo pamoja na serikali kuleta mpango wa mradi wa Kigoma Joints Program(KJP)ulioanza mwaka 2017 na kuisha 2021 mpango huu unashirikisha katika maeneo ya afya,Elimu,Unyanyasaji wa kijinsia,mazingira.

"Mpango huu utasaidia kuendelea mkoa wetu wa Kigoma kwenye hizo nyanja ambazo zinagusa"alisema.Naye muelimishaji maswala ya kijinsia kutoka asasi ya kividea Vitalis Cosmas alisema kuna ushirikiano mdogo wa mwendelezo wa ufuatiliaji kwa wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
 Mratibu wa mashirika.ya wa umoja wa mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez akipanda mti wa kumbukumbu nje ya ofisi ya dawati la kijinsia la Polisi Kigoma iliyojengwa kupitia mradi wa Kigoma Joints Program(KJP)
 Mkuu wa Mkoa Kigoma brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa maelekezo kwa mafundi wanaojenga vizimba vya kuuzia katika soko la Kasulu linalojengwa kupitia mradi wa Kigoma pamoja

Ujenzi wa vizimba vya kuuzia kwa ufadhili wa mradi wa Kigoma pamoja katika soko la Kasulu unaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...